Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) unawakaribisha wananchi wote kutembelea katika banda lao ili kupata huduma kwenye maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Wakulima yanayofanyika mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale almaarufu kama viwanja vya nanenane. Huduma zinazopatikana katika banda la RITA ni Usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watu wote waliozaliwa Tanzania bara, elimu kwa umma kuhusu usajili wa Ndoa na Talaka, Ufilisi na Udhamini pamoja na huduma ya msaada wa kisheria kuhusu masuala ya Wosia na Mirathi. 

Akizungumza Afisa Usajili Msaidizi wa RITA, Bi. Noela G. Ituga anasema kuwa "tunapenda kuwakaribisha sana wananchi wote wafike katika banda letu ili kufaidika na huduma zetu kwa urahisi kabisa ambapo pia tunasajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa hapahapa viwanjani kwa kila mtu aliyezaliwa Tanzania bara hivyo basi wakulima na watanzania wote wasiokuwa na vyeti hivi muhimu watembelee katika banda la RITA kupata huduma zetu".

Maonesho haya yameanza tarehe 01 mwezi wa Nane mwaka 2022 na yanatarajiwa kufikia kilele tarehe nane ambapo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale almaarufu viwanja vya nanenane mkoani Mbeya na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mheshimiwa Rais Samia Suluhu.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...