Ankara, Uturuki

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi na Naibu Waziri  wa Afya wa Uturuki Dkt. Tolga Tolunary wamekutana na kufanya mazungumzo ya namna ya kuanza mara moja utekelezaji wa Mkataba wa mashirkiano katika sekta ya afya yaliyosainiwa mwaka 2017.

Majadiliano hayo yamefanyika  Leo tarehe 8/8/2022 katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Ankara, Uturuki.

Maeneo mbalimbali ya ushirikiano yalijadiliwa ikiwemo mafunzo ya kibingwa na ubingwa ubobezi kwa wataalamu wa kada mbalimbali za Afya, matibabu yasiyopatikana nchini Tanzania, uwekezaji wa Hospitali, viwanda na vifaa tiba nchini Tanzania, mageuzi ya mfumo wa TEHAMA wa taarifa za afya za wananchi wote unavyotumika nchini humo.

Katibu Mkuu pamoja na ujumbe aliombatana nao walipata fursa ya kuelezwa kuhusu mageuzi yaliyofanyika  kwa miaka ishirini sasa katika mfumo wa sekta ya afya na uendeshaji wa bima ya afya kwa wote unavyotekelezwa nchini Uturuki.

Aidha, uzoefu ulitolewa wa matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika kuwa na e-Database ya wagonjwa wote nchini humo, utunzaji na  usafirishwaji wa kumbukumbu zao (vipimo, magonjwa, dawa) kutoka hospitali moja kwenda hospitali nyingine na utambuzi, ufatiliaji(tracking) na udhibiti wa dawa katika supply chain kuanzia ngazi ya utengenezaji/uingizaji mpaka kwa mlaji (mgonjwa).

Vilevile, Katibu Mkuu na ujumbe wake walielezwa kuhusu mfumo unaotumiwa na Wizara ya afya kwenye huduma za dharura na majanga ambapo magari yote ya dharura yanaratibiwa kutoka vituo mbalimbali katika kituo kikuu kilichopo wizarani pamoja na uwepo wa mfumo unaofuatilia magari ya kubeba wagonjwa (ambulances) nchi nzima.

Viongozi hao walikubaliana kuundwa kwa kamati maalum ya kiutendaji itakayoratibu makubaliano yaliyofikiwa na kuweka mfumo wa tathimini na ufuatiliaji wake.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu pia aliambatana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Hassan Mwamweta na kutoa salaam za Mheshimiwa  Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu kwa Serikali ya Uturuki.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...