NA FARIDA SAID, MOROGORO.
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeibuka mshindi wa kwanza kwenye kundi la vyuo vikuu na vyuo vya kati kwenye maonesho ya nanenane kanda ya mashariki yaliofanyika mkoani morogoro na wa pili kwa kundi la washriki wa jumla katika kanda hiyo.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa ushindi huo Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya elimu ya kujiendeleza Prof.Dismas Mwaseba alisema wamefurahishwa na ushindi huo na wanajipanga kwa maonesho yanayofuata ili kupata ushindi kwa mara nyingine.
“Leo kwetu ni siku ya furaha kubwa kupata ushindi wa pili kwa mshindi wa jumla na ushindi wa kwanza kwa taasisi zilizoshiriki maoneosho haya, nitoe pongezi kwa watumishi wote wa SUA walioshiriki katika kuonesha teknolojia mbalimbali kwenye viwanja hivi na kuifanya SUA kuibuka kidedea.” Alisema Prof. Mwaseba
Aidha alisema wanaenda kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika maonesho ya mwaka huu ili mwaka unaofuata waweze kushika nafasi ya kwanza kwenye maonesho hayo.
Alisema ushindi huo umechangiwa na teknolojia mbalimbali ambazo SUA imezionesha katika maonesho hayo ikiwemo vipandwa vya mazao mbalimbali, mifugo, mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia simu ya mkononi pamoja na ndege isiyo na rubani(Drone ) inayomsadia mkulima kukagua shamba kwa kupiga picha na kuona maendele ya shamba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...