NA FARIDA SAID, MOROGORO

Watanzania wametakiwa kuacha tabia ya kutupa taka ngumu na hatarishi ovyo kwenye maeneo yao badala wake wazihifadhi na wafuate utaratibu wa kuteketeza taka unaotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kutunza mazingira.

Imeelezwa utupaji taka ovyo hasa wa chupa za plastiki,vyuma pamoja na vifungashio vya dawa za kuulia wadudu na mbolea umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa uchafunzi wa mazingira hususani katika mito.

Hayo yameelezwa na Mchumi kilimo kutoka mfuko wa uhifadhi wa wanyampori afrika( African wildlife foundation –AWF) Bwana Alexander Mpwaga kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji nanenane kanda ya Mashariki alipo kuwa natoa elimu kwa wananchi juu ya uhimu ya matumizi ya KIZIMBA cha kuhifadhia taka.

Alisema kizimba ni sehemu ya kuhifadhia taka hatarishi zinazoweza kuwa na kemikali yeyote ambayo inaweza kusababisha madhara kwenye mazingira kama chupa za plastiki zilizohifadhia dawa ya kuulia wadudu, mbolea pamoja na vifungashio vingine vinavyotumika kwenye shughuli za kilimo,mifugo na uvuvi.

Alisema ni vyema watanzania wakawa na utamaduni wa kuhifadhi taka hizo kwenye vizimba vya aina yeyote ambavyo wanaweza kuvitengeneza kwenye maeneo yao kwani vinasaidia katika utunzaji wa mazingira, afya za binaadamu, wanyama pamoja na viumbe hai vya majini.

“Hivi vizimba tukivitumia vizuri katika kuhifadhi taka hatarishi vitatusaidia katika kutunza mazingira yetu kwani kuna wakulima wanatupa ovyo chupa za dawa zenye sumu kwenye vyanzo vya maji bila ya kujua kwawa wanaharibu mazingira na kuadhili viumbe vya majini pamoja na binadamu wanaotumia maji katika mito hiyo.”alisema Alexander

Pia alisema pamoja na kuhifadhi mazingira pia kizimba kinaweza kuwa chanzo cha mapato kwa vijana kwa kukusanya chupa za plastiki za maji ya kunywa na kuziuza kwenye viwanda kama malighafi ya kutengeneza biadhaa nyingine

Akizungumza kwenye maonesho ya nanenane mara baada ya kuona teknolojia mbalimbali za kilimo na ufugaji Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi CCM), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amewapongeza AWF kwa kusirikiana na SAGCOT pamoja na wadau wengine kwa kuchagiza utunzaji wa mazingira hususani kwenye sekta ya kilimo katika bonde la mto kilombero na maeneo mengine.


Shaka alisema kwenye maonesho ya mwaka huu ameshudia mabadiliko na maboresho makubwa na yote yanaonesha utayari wa viongozi katika kutafsiri dhana na dhima waliyonayo kwa vitendo ya kusimamia maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kilimo, mifugo na uvuvi.


Mkulima wa mpunga kutoka skimu ya umwagiliaji ya Itete Bi. Pendo Lusamba ikieleza umuhimu wa kufunga bidhaa kwenye vifungashio maalumu hasa mchele.




Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi CCM), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akikagua kizimba cha kuhifadhia taka hatarishi alipotembelea bada la SAGCOT kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki mkaoni Morogoro.
Mchumi kilimo kutoka mfuko wa uhifadhi wa wanyampori afrika( African wildlife foundation –AWF) Bwana Alexander Mpwaga akitoa maelezo kuhusu mradi wa kizimba unavyowasaidia wananchi katika kuhifadhi kwenye maonesho ya nanenane kanda ya mashariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...