Afisa Biashara Mwandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Doto Ditteba akielezea namna usajili wa wakulima unavyopaswa kufanyika kwa viongozi wa kijiji cha Godima wilayani Chunya Mkoani Mbeya tarehe 5 Agosti, 2022.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Happinesess Mbelle akizungumza jambo wakati wa kikao kifupi baina ya viongozi wa TFRA walipopita kuangalia mwenendo wa usajili wa wakulima katika kijiji cha Godima Wilayani Chunya tarehe 5 Agosti, 2022. Kushoto kwake ni Afisa Biashara Mwandamizi wa TFRA, Doto Detteba.
Wakulima wa kijiji cha Chokaa wilayani Chunya wakisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Uagizaji na uuzaji mbolea  nje ya Nchi, Louis Kasera (hayupo pichani) alipotembelea pamoja na wataalam wengine kujionea mwenendo wa usajili wa wakulima kabla ya kuanza kutoa mbolea za ruzuku.

KUFUATIA utekelezaji wa taratibu za utoaji wa mbolea za ruzuku tayari wakulima 500 wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamesajiliwa ili kunufaika na ruzuku ya mbolea itakayotolewa msimu ujao wa kilimo.

Hayo yalibainika wakati wa ziara ya watendaji wa Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) walipotembelea wilaya hiyo ili kujionea mwenendo mzima wa usajili wa wakulima.

Akizungumza katika vituo mbalimbali vilivyokuwa vikisajili wakulima Meneja Uagizaji na uuzaji mbolea nje ya Nchi, Louis Kasera aliwataka wakulima waliosajiliwa kuwa mabalozi kwa wakulima wengine ili wafike kujisajili.


"Hakuna mbolea ya ruzuku pasipo kusajiliwa" alikazia Kasera na kuongeza kuwa utaratibu wa kusajili wakulima umeanza mapema ili ufikapo msimu kilimo wakulima waweze kupatabidhaa hiyo kwa wakati.

Kwa upande wake, Afisa Biashara Mwandamizi, Doto Diteba, alisema ukusanyaji wa taarifa za idadi ya wakulima na ukubwa wa mashamba wanayoyamiliki zitaisaidia serikali kujua idadi ya wakulima wanaopatikana katika eneo hilo na kiasi cha mbolea kitakachohitajika kulingana na ukubwa wa mashamba yanayomilikiwa na wakulima wa eneo husika.

Ameongeza kuwa ni sharti shamba moja limilikiwe na mtu mmoja na si kila mwanafamilia kujisajili kwa kutoa taarifa za shamba moja.

Kwa upande wake, Elius Mtware Mjumbe halmashauri ya kijiji cha Godima Wilayani Chunya ameishukuru serikali kwa kwawakumbuka wananchi kutokana na hali duni walizonazo utoaji wa mbolea za ruzuku utawasaidia kuzalisha kwa tija.

Aidha ameiomba serikali kutoa msaada kupata ruzuku hata kwa pembejeo nyingine za kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao wanayolima.

Usajili wa wakulima ni moja ya mikakati ya kudhibiti utoaji wa mbolea za ruzuku kwa mwaka huu wa fedha ili kuhakikisha wakulima halisi wananufaika na mbolea za ruzuku na kusababisha uwepo wa chakula nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...