Meneja  Huduma za Hali ya Hewa Kilimo Isac Yonah akizungumza na waandishi wa habari  katika mtambo wa kuangalia hali ya hewa katika maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea  katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Meneja  Huduma za Hali ya Hewa Kilimo Isac Yonah akizungumza na waandishi wa wa habari namna wanavyopokea taarifa za hali ya hewa kutoka katika mtambo wa kuangalia hali ya hewa , maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea  katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Meneja wa Kanda ya Mbeya wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Abel Nyamenda akionesha waandishi wa habari namna utabiri unavyoafanyika kwenye banda la TMA katika  Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea  viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

*Kutafanya kuwa na elimu ya namna bora kulima kutokana na utabiri huo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV , Mbeya
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuwa kuwepo kwa mamlaka hiyo inasaidia wakulima kuweza kujua msimu wa kuanza kulima kwa kujua hali ya mvua na pamoja na mazao gani yanayaweza kuendana na mvua hizo.

Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye maonesho ya Kilimo Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya Meneja Huduma za Hali ya Hewa Kilimo Isack Yonah amesema kuwa wananchi wanatakiwa kufatilia masuala ya hali ya hewa kwani ndio inafanya kwao kujiandaa katika masuala ya kilimo.

Amesema taarifa za hali hewa hazina mpaka kutokana na kupata taarifa mbalimbali duniani ambazo zinasaidia kuwapa wananchi taarifa za hewa hizo.

Amesema kuwa katika taarifa za msimu wa kilimo zinatoka kuanzia mwezi Septemba ambapo kwa wakulima wanatakiwa kufatilia ili kuweza kuanza kujiandaa na kilimo na kujua kiwango cha mvua kitachokuwepo.

Amesema kuwa serikali imedhamiria kuendelea kuwekeza katika rada ili kuendelea kuboresha utabiri kutokana na teknolojia inavyokwenda katika sekta hiyo.

Aidha amesema kuwa wananchi wenye uwezo wanaweza kuwekeza katika utabiri wa hali ya hewa na TMA kusimamia ubora wa mitambo na wataalam walionao katika kutabiri hali ya hewa.

Yonah amesema wananchi wajitokeze katika kutembelea banda la TMA kuweza kupata taarifa mbalimbali pamoja na elimu kuhusiana na utabiri wa hali ya hewa unavyofanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...