Baadhi ya wakulima na wafanyabiashara ya mbolea wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) Kanda ya Ziwa, walipotembelea banda lao lililopo katika maonyesho ya nanenane kwa mikoa ya kanda ya ziwa inayofanyika katika viwanja vya Nyamhongolo mkoani Mwanza.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA), Kanda ya Ziwa imewataka wananchi kutoka mikoa yote ya kanda ya ziwa kufika katika ofisi za mitaa ili kujiandikisha kwaajili ya kunufaika na mbolea ya ruzuku.
Akizungumza na Michuzi Blog katika maonyesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Ziwa, Kaimu Meneja wa mamlaka hiyo kanda ya ziwa, Hanafi Mohamed amesema kuwa Serikali imetoa Sh 150 kwa ajili ya ruzuku ya mbolea hivyo kuwataka wakulima kuchangamkia ruzuku hizo.
“Mbolea ipo tayari kwa sasa japokuwa katika kanda ya ziwa tunatarajia kuwasilisha vitabu vya kujiandikisha ndani ya wiki moja hivyo jiandaene kupokea mbolea hiyo ili kuboresha kilimo,” amesema.
Ameongeza kuwa vitabu hivyo vya kujisajili vitatolewa katika ofisi za Serikali za mitaa ambapo kila mkulima ataenda kujiorodhesha ili kunufaika na mbolea hiyo.
Kuhusu wauzaji haramu wa mbolea katika maduka mbalimbali, ametaka kujisajili na kupata leseni ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.
“Muuzaji wa mbolea ambaye hana leseni anatakiwa kufika katika ofisi za TFRA akiwa na TIN namba au cheti cha kampuni kinacholewa na BRELA kwa ajili ya kujaza fomu na kupatiwa leseni,” ameongeza.
Akifungua maadhimisho ya nane nane mkoani Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima akawataka wakulima kutumia fursa za elimu ya kilimo na masuala mengine zinazopatikana katika maonyesho ya nanenane ili kumudu kilimo na ufugaji katika njia na mifumo ya kisasa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...