MAMLAKA ya mapato mkoa Mbeya (TRA) imesema kuwa kumekuwa na ongozeko la ulipaji kodi kwa hiyari hasa upande wa kilimo kutokana na kutatua migogoro nje ya mahakama.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya mapato Mkoa wa Mbeya(TRA), Nuhu Suleiman wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati waliyoweka kwa walipa kodi katika kipindi hichi cha maonyesho ya wakulima Nanenane ambayo kitaifa inafanyika mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale Jijini hapa.

Suleiman amesema kuwa kitu kingine kinacholeta msukumo wa hiyari kwenye ulipaji kodi ni usikilizaji wa malalamiko kwa walipa kodi.

“Ni kweli suala la kodi linahusu kila mwananchi na wakati mwingine kuna kuwa na changamoto ya nguvu kazi lakini sasa hivi tunaishukuru serikali na pia tunashukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwasababu tumeongozewa watumishi 2000 kwa hiyo sisi watumishi tumejipanga kwenda maeneo ambayo yamejitenga na mji kwa ajili kusambaza elimu”amesema.

Aidha Kaimu Meneja huyo amesema kuwa katika maonyesho hayo pia kutakuwa na fursa kwa wawekezaji kuweza kuelewa bidhaa ambazo zipo kwenye misamaha ya kodi.

Hata hivyo Suleiman amesema kwa suala la kodi ni muhimu na kwamba nchi haiwezi kwenda bila ulipaji wa kodi hivyo elimu itaendelea kutolewa kwa wananchi ili waweze kuendelea kulipa kodi.

Fatuma Mohamed ni mjasiliamali wa Duka la Nguo Soweto amesema hivi sasa ulipaji wa kodi unaenda heshima kubwa sana kwani tunalalamika wenyewe.

“Wengi tumebadilika kutokana na TRA kutoa elimu mara kwa wananchi ndo unakuta hata kwenye maonyesho tunajitokeza kwa wingi.” Amesema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...