BAADA ya haki ya uhai, haki inayofuata ni haki ya kupata habari na suala la habari halihitaji mipaka ya nchi.

Ni kauli ya Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) akizungumza katika Kipindi cha Mezani kinachorushwa na Kituo cha Redio cha EFM, jijini Dar es Salaam leo.
 

Balile amesema, haki ya uhai haipo kwenye mikono ya mwanadamu yeyote lakini haki ya habari inapangwa na wanadamu namna ya kuitumia.

“Tunataka sheria hizi za habari zitupe mwongozo wa msingi. Baada ya haki ya uhai, kinachofuata ni haki ya kupata habari,” amesema Balile wakati akizungumzia mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari nchini.
 

Amesema kwamba, duniani kuna mifumo mitatu ya usimamizi wa vyombo vya habari, ambapo kila Serikali huamua kuchagua mfumo mmoja kati ya hiyo.

“Kuna mfumo wa kwanza ni self regulation (kujitathmini), mfumo wa pili ni Serikali kushika vyombo vya habari kama ilivyo sasa na mfumo wa tatu ni co-regulation ambapo Serikali na wadau wa habari wanakuwa na chombo ambacho kinawaunganisha.

“Sisi tunataka huu mfumo wa tatu ambao ndio tunaupigania, sio ule wa serikali kuwa mlalamikaji, msuluhishi na hakimu. Huu mfumo utazikwa kwa kuunda Baraza la Huru la Vyombo vya Habari,” amesema Balile katika Kipindi cha Mezani kinachorushwa na Kituo cha Redio cha EFM, jijini Dar es Salaam leo.

Amesema, TEF kwa kushirikiana na wadau wa habari nchini, wanapendelea mfumo wa tatu ambao unatoa fursa kwa pande zote mbili (wadau na serikali) kuwa na sehemu ya kukutana pale kunapokuwa na malalamiko.

Akizungumzia ushirikishwaji wa wanahabari wenyewe kwenye mabadiliko hayo, Balile amesema wamekuwa na mikutano ya mara kwa mara na wanahabari katika kuwafafanulia vifungu hivyo.Na kwamba, TEF imekuwa ikifanya mikutano na wahariri, waandishi pamoja na waandishi wa habari za mtandaoni (online contents.)

“Vikao hivi tumevifanya mara kwa mara na waandishi wanaelewa, na hatua iliyopo sasa ni kwenda kwenye mjadala ulioitishwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari tarehe 11 – 12 Agosti mwaka huu kwa ajili ya kupitia vifungu vinavyolalamikiwa,” amesema.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...