Mkurugenzi wa huduma za Tiba, Omary Ubuguyu, akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 5, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Global HOPE programu itakayowajengea uwezo wataalamu wa kutibu saratani ya damu kwa watoto.

Dkt. David Poplack ambaye ni Profesa wa magonjwa ya saratani kwa watoto na Mkurugenzi wa Global HOPE program kutoka hospitali ya watoto ya Texas nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Global HOPE programu itakayowajengea uwezo wataalamu wa kutibu saratani ya damu kwa watoto.

 

CHUO  Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kushirikiana na Global HOPE Programu ya Texas Marekani, wamefungua programu itakayokuwa ikifundisha madaktari katika uzamivu na uzamili  kwa matibabu yanayohusu saratani ya damu kwa watoto hapa Tanzania.

Programu hiyo pia itasaidia kuongeza nafasi ya watoto wenye saratani ya damu na zingine kuishi muda mrefu na kupona kabisa ugonjwa huo tofauti na sasa ambapo wengi wamekuwa wakifariki.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya, wakati wa ufunguzi wa programu hiyo leo Agosti 5,2021 jijini Dar es Salaam,  mkurugenzi wa huduma za tiba Omary  Ubuguyu amesema, programu hiyo itawajengea uwezo madaktari wa kutambua kutibu na kuongeza upatikanaji wa dawa kwa Watoto wenye saratani ya damu na magonjwa mengine ya damu

"Programu hii  itafanya kazi katika maeneo makuu manne, kutoa mafunzo kwa ajili ya wataalamu kuwajengea uwezo wa kutambua kutibu na kuongeza upatikanaji wa dawa kwa Watoto wenye saratani na magonjwa mengine ya damu.

Pia itarahisisha upatikanaji wa dawa kwani kuna baadhi ya dawa zilikuwa zinapatikana kwa changamoto lakini sasa programu hiyo itakwenda kuongeza nafasi ya upatikanaji wa dawa hizo,  vipimo na uwezo wa kutambua ugonjwa mapema zaidi na uboresha miundombinu ya kutolea huduma.


hivyo baada ya kuanza kwa programu hii tunategemea baadhi ya hospitali ambazo zitachaguliwa zitaweza kutoa huduma bora na za kibingwa katika masuala ya saratani na damu kwa waototokujenga uelewa kwa jamii kuhusiana na saratani na magonjwa mengine ya damu haswa kwa watoto.


Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)  Profesa Andrea Pembe amesema, mwaka 2020 waliingia mkataba wa makubaliano na Global HOPE ili kuweza kuboresha ufundishaji na kuongeza wataalamu ambao watakuwa wanatibu saratani ya damu kwa watoto

Amesema,  lengo kubwa  ni kuhakikisha kwamba watoto  wengi waweze kuishi kwa matumaini zaidi wakiwa na tabasamu la maisha kwa kupunguza uzito wa ugonjwa na pale inapowezekana waweze kupona kabisa wasiwe na ugonjwa wowote.

"Mpaka sasa kuna wataalamu sita ambao wako kwenye kwenye mafunzo, watatu wameishamaliza na watatu wanamaliza mwaka huu mafunzo yao". Amesema Pembe

"Tumekuwa katika mpango ambao utapelekea tuweze kuzalisha wataalamu wa afya huku wakati huo huo tukifanya tafiti ambazo zitaboresha matibabu kwa watoto wenye magonjwa ya saratani ya damu na kuongeza zaidi huduma katika nchi yetu mpaka kufikia kwenye ngazi za mikoa na wilaya". Amesema

Dkt. Lulu Chirande, Daktari bobezi wa magonjwa yùa saratani na damu kwa watoto na mhadhiri Mwandamizi MUHAS, amesema tatizo la saratani ya damu kwa watoto ni kubwa sana, siyo hapa nchini tu bali ulimwenguni kote ambapo inakadiriwa watoto zaidi ya laki tatu wanapata saratani.

Amesema, kwa hapa Tanzania watoto wale wanaofanikiwa kufika hospitali ni sehemu ndogo ya watoto wanaopata saratani huku wengi wao wakifariki kabla hata ya kufanyiwa utafiti wakaambiwa wanasaratani kwani asilimia kubwa hawafanikiwa kufika katika hospitali zenye utaalamu wa kutosha na hivyo wanafariki katika hospitali za Chini na wengine bila hata ya kufika hospitali kwa ajili ya kutogundulika walikuwa na tatizo gani.

"Kuna kama watoto 800 kila mwaka ambao wanapata saratani na wanafika hospitali ambapo wanaweza kuchunguzwa na kuambiwa wana saratani...,hapa Muhimbili kila mwaka tunapata wastani wa watoto 500 wapya ambao wanagundulika kuwa na tatizo hilo. Amesema Dkt. Chirande.

unaweza kusema asilimia 60 na zaidi ya watoto tunaowatibu sisi wako katika hatua ya tatu na ya nne, wa kwenye hatu ya kwanza huwa hata hatuwaoni , hatua hizo zikishafika ni vigumu sana kwa mtoto kutibiwa na kupona, mtoto mwenye saratani hatua ya nne hata kama angekuwa anatibiwa Marekani uwezekano wake wa kupona ni mdogo sana.


Ameongeza kuwa, changamoto zilizopo ni kwamba dalili za saratani nyingi ukiondoa zile zenye vivimbe inafanana na magonjwa mengi sana, zile zenye vivimbe kwa kuwa i ukiwa nje utaona ila ukiwa ndani huwezi kuona. Ila mtoto anaanza na dalili za kawaida, homa, kulegea homa mara kwa mara, kupungukiwa damu lakini utafiti haufanyiki kwa nini anapungukiwa damu.

"Saratani za watoto nyingi zinakuwa na dalili za magonjwa mengine,  hivyo mzazi akiona mtoto anaumwa ni vema akamuwahisha kituo cha afya hivyo katika vituo hivyo watia huduma wanatakiwa wawe na uelewa kugundua kuwa kuna saratani utafiti unaonyesha kuwa wazazi wanawahi kuwapeleka watoto hospitali ama dispensary huko waliko lakini kutoka hapo inachukua wastani wa miezi minne  mpaka sita hajulikani kama anasaratani.


sasa wanaofanikiwa kugundulika ni wale ambao wana aina za saratani ambazo zinakuwa taratibu wale wenye saratani ambazo ni kali sana zinaenda haraka wakiwa hawana miezi sita bila matibabu wanakufa njiani wakiwa wanatafuta huduma.

Amesema chanzo cha saratani kwa watoto siyo kimoja kwani asilimia 90 za idadi ya wa watoto wanaopata saratani huwezi kusema imesababishwa na nini,  watu wazima waaambiwa ni mfumo wa maisha tunavyokula, uvutaji sigara unywaji wa pombe nk. Lakini Kuna watoto anapata saratani anamiezi miwili.


Ameongeza kuna asilimia kama tano ya watoto wanaopata saratani ndio  unaweza kusema imesababishwa na nini lakini nyingine yote haijulikani.  Hivyo basi vita juu saratani ya watoto siyo kujua visababishi bali ni kuwagundua mapema sana, na wakigundulika mapema wanatibiwa na wanapona kwai mtoto mwenye saratani hatua ya pili matibabu yake ni mafupi na anakuwa amepona lakini mwenye hatua nne matibabu yake ni magumu sana na ugonjwa unakuwa umeishakuwa mkubwa unahitaji kumtibu kwa muda mrefu.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Andrea Pembe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Global HOPE programu itakayowajengea uwezo wataalamu wa kutibu saratani ya damu kwa watoto.

Daktari bobezi wa magonjwa ya saratani na damu kwa watoto na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Muhimbili, dkt. Lulu Chirande akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Global HOPE programu itakayowajengea uwezo wataalamu wa kutibu saratani ya damu kwa watoto.Daktari bobezi wa magonjwa ya saratani na damu kwa watoto na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Muhimbili, dkt. Lulu Chirande akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Global HOPE programu itakayowajengea uwezo wataalamu wa kutibu saratani ya damu kwa watoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...