Mwalimu wa Chuo cha VETA Chang'ombe, Ally Issa akionesha mbolea ya asili ya kupandia na kukuuzia ambayo kwa lita moja ni robo Ekari ambayo imekuwa na wahitaji wengi katika maonesho ya Kilimo Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mwananchi akitumia kifaa cha kupukuchia mahindi kilichobuniwa wa VETA Chang'ombe ambayo inaenda kuondoa changamoto ya kutumia miti kwa kupiga mahindi, kwenye maonesho ya Kilimo Kitaifa yanayofanyika viwanja vya John Mwakangale, Jijini Mbeya.



Wananchi wakiwa katika banda la VETA kuangalia ubunifu wa Teknolojia katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane 2022 jijini Mbeya.

*Inatumika kukuuzia na kupandia mimea

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika maonesho ya kilimo imekuja na teknolojia za kilimo zitakazo msaidia mkulima na mfungaji kuzalisha kwa ufanisi wa mazao na mifungo.

Katika moja ya ubunifu huo ni pamoja na kuwa mbolea ya asili ambayo imebuniwa na Mtaalam wa Maabara wa VETA Chang'ombe Ally Issa amesema mbolea hiyo inatumika katika kukuzia na kupandia bila kuathiri udongo kupoteza rutuba.

Amesema kuwa matumizi ya mbolea ya viwandani yanachangia katika kufanya mashamba kudumaa katika uzalishaji lakini mbolea ya asili inafanya shamba kuendelea kuzalisha.

Aidha amesema mbolea ya asili ya maji kwa lita moja inatumika kupandia na kukuuzia kwa nusu ekari ya shamba.

Amesema amebuni hiyo mbolea kutokana na bei ya mbolea kupanda hivyo mbolea hiyo itasidia wakulima kupunguza gharama za mbolea.
Katika upande mwingine mbunifu amekuja na teknolojia ya mashine ya kutengeneza chakula cha samaki ambapo wafugaji wa wa samaki watazalisha samaki wengi kutokana na chakula hicho kuchanganywa pamoja.

Mbunifu wa Kifaa hicho Mwalimu wa VETA Songea Sozaki Mbulu amesema kuwa wafugaji wamekuwa na changamoto ya ulishaji samaki katika kuweka mchanganyiko wa chakula.

Mwalimu wa VETA Chang'ombe Kilanga Kintu amebuni mashine ya kupukua mahindi ambayo mtu mmoja anaweza kupuchua mahindi tano kwa siku na kuachana kupiga kwa kwa fimbo ambapo yanafanya mahindi kukosa ubora.

Amesema mahindi wakati mwingine yanakosa ubora wa soko kutokana na namna ya upikuchaji wa mahindi hayo hivyo mashine hiyo ni kutumia mikono kwa kuzungusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...