Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dk.Stephan Ngailo akiwahudumia wananchi waliotembelea banda la TFRA kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Matlida Kassanga akiwahudumia wananchi waliotembelea banda la TFRA kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)Dkt. Stephan Ngailo amesema kuwa wananchi wamekuwa na mwitikio katika kujua hali ya mbolea nchini utakapoaza Msimu wa Kilimo kwa mwaka 2022/2023.

Dkt.Ngailo ameyasema hayo katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale , Jijini Mbeya.

Amesema wananchi katika kanda za nyanda za Juu Kusini wenye mikoa saba ambayo Ruvuma , Iringa, Njombe , Mbeya, Songwe, Rukwa pamoja na Katavi wananchi wamefunga safari kupata taarifa za mbolea.

Dkt.Ngailo amesema kuwa mwitikio huo mzuri kwani kama wadhibiti mbolea ni wajibu kutoa majawabu ya kuwatoa hofu juu ya suala la mbolea.

Amesema kuwa moja ya swali linaloulizwa ni suala la mbolea ya Ruzuku ambapo kazi yao ni kuendelea kutoa utaratibu utaotumika katika kupata mbolea kwa bei nafuu kutokana na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Hassan Suluhu kuona namna bora ya kusaidia wakulima ili kuzalisha chakula kwa wingi.

Hata hivyo amesema kuwa Serikali haitaishia katika kutoa Bilioni 150 kwani itaendelea kutoa ruzuku hiyo kutokana na mahitaji ya wakulima wakati wa msimu wa kilimo utakapoanza.

"Tutaendelea kutoa elimu kwa wananchi wetu katika kuondoa changamoto wakati wa msimu wa kilimo utakapofika kwa kuweka uwazi wa mbolea ya ruzuku." amesema Dkt.Ngailo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...