
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka
Watanzania waendelee kuwa wazalendo kwa Taifa lao na washirikiane na Serikali
katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Ametoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Agosti 05, 2022) wakati akizungumza na wakazi wa
Ikungi alipokuwa katika ziara ya kikazi kataka wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
“Nataka niwasihi
msikwamishe maendeleo, lazima kila mmoja awe na uzalendo na wilaya yake, nawapongeza
madiwani kwa mpango wenu wa kupanga mji huu.”
Waziri Mkuu alisema halmashauri
ya wilaya hiyo imeweka mpango wa kuendeleza mji wake, wananchi ambao maeneo yao
yatachukuliwa kupisha mradi huo watafidiwa kulingana na taratibu za uthamini.
Alisema Mthamini wa
Serikali ana vigezo vya fidia, hivyo aliwasihi wananchi hao kuacha tabia ya
kukataa kila mthamini anayekwenda kufanya uthamini katika eneo lao.
“Lazima mthamini mipango
ya halmashauri yenu ya kuuboresha mji huu, isitokee mtu mmoja au wawili
wakakwamisha maendeleo ya wenzao wa wilaya nzima.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...