Na Janeth Raphael
SERIKALI imesemaa hadi kufikia septemba 5.2022 kiwango cha kaya zilizohesabiwa nchi nzima na taarifa za kidemografia,kiuchumi na mazingira yake zimekusanywa kwa asilimia 99.99 na sensa ya majengo ni asilimia 99.87 ya majengo yote nchini.
Akitoa taarifa kuhusu tathmini ya zoezi la sensa ya watu na makazi,sense ya majengo na sense ya anwani za makazi kwa mwaka 2022,kamisaa wa sensa Tanzania bara Anne makinda ambaye ni spika mstaafu wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, amesema zoezi la sensa kwa mwaka huu limekamilika rasmi kwa asilimia 99.99 ambapo sensa ya majengo ni asilimia 99.87 ambapo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania samia suluhu hassan atatangaza october 2022.
’’napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wananchi wote kwa ushirikiano wenu wakati wa kutenga maeneo ya kuhesabia watu na wkati wa zoezi la kuhesbu watu,pia nawashukuru viongozi katika ngazi zote kuanzia ngazi ya taifa hadi mtaa/kitongoji/shehia kwa jitihada zao na ushirikiano wao wakati wote wa kukamilisha awamu hiiya utekelezaji wa sensa’’ amesema Anne makinda.
Aidha amesema kuwa awamu ya pili ya utekelezaji wa sensa imekamilika na sasa wanaingia awamu ya tatu ambayo ni muhimu na inajumuisha shughuli zote za baada ya kuhesabiwa watu.
“Tumekamilisha awamu ya pili ya utekelezaji wa sense,sasa tumeingia awamu ya tatu ambayo ni ya muhimu sana na inajumuisha shughuli zote baada ya kuhesabu watu,na shughuli hizo ni pamoja na uchambuzi wa taarifa za sense,uzinduzi rasmi wa matokeo ya mwanzo ya sense na usambazaji wa matokeo ya sensa,ambapo taarifa ya mwanzo itahusu iadi ya watu waliohesabiwa nchi nzima na kwajinsia zao katika ngazi zote za utawala na matokeo haya yatatolewa mwezi oktoba mwaka 2022 na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania samia suluhu hassan’’ amesema Anne Makinda.
Kwaupande wake kamisaa wa sensa zanzibar balozi mohamed hajji Hamza amesema sensa hii imefanyika kidigital kwakutumia wataalam wa ndani na imefanyika kwa ustadi mkubwa na ubora wa hali ya juu.
Naye mtakwimu mkuu wa serikali dkt. Albina Chuwa amesema asilimia ya watu ambao hawajahesabiwa, kisayansi asilima 0.01 ni wale watakaokuja kuhesabiwa sensa ya awamu ijayo na haiathiri katika kupanga maendeleo ya Nchi huku akibainisha kuwa sensa ya majengo ni endelevu.
Home
HABARI
99% YA KAYA NCHI NZIMA NA TAARIFA ZA KIDEMOGRAFIA, KIUCHUMI NA MAZINGIRA YAKE ZIMEKUSANYWA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...