Na Englibert Kayombo – WAF, Dar Es Salaam.
Waziri
wa Afya Mhe Ummy Mwalimu leo amefanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa
Global Fund Bw. Peter Sands kuhusu uboreshaji wa huduma za afya nchini
kupitia miradi ya Global Fund inayotekelezwa hapa nchini.
Waziri
Ummy ameishukuru Global Fund kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Mapambano dhibi ya Ugonjwa wa Virusi vya
Ukimwi, Kifua Kikuu pamoja na Malaria.
Amesema Serikali ya Awamu
ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imelenga kuboresha ubora wa
huduma hivyo kwa kushirikiana na Global Fund Serikali inatarajia kufikia
malengo yake katika mapambano dhidi ya VVU kwa kuwa na afua zilizolenga
kuelimisha na kuhamasisha wananchi kutambua mapema hali za afya zao,
kuongeza utambuzi wa watu wapya wenye VVU, pamoja na kuzuia maambukizi
mapya kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto.
Waziri Ummy ameishukuru
Global fund kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa
afua mbalimbali zinazolenga kukabiliana na magonjwa mengineyo yakiwemo
Kifua Kikuu, Malaria UVIKO-19 ikiwa pamoja na uboreshaji wa mifumo ya
Sekta ya Afya nchini.
Kwa upande wake Bw. Peter Sands,
ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha Sekta ya Afya nchini na
kutoa kipambuele katika mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi, Malaria na
Kifua Kikuu.
Bw. Sand ameahidi ushirikiano zaidi na kuendelea
kufanya kazi kwa karibu na Tanzania kufikia malengo ya Kidunia na
kukabiliana na maradhi hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...