Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York na kuwataka kutanguliza uzalendo na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa faida ya nchi.
Balozi Mulamula pia amewataka watumishi hao kusimamia matumizi mazuri ya fedha za Serikali katika kutekeleza majukumu yao kwenye vituo vya uwalikishi wa nchi na kutangaza kazi mbalimbli zinazofanywa na ubalozi ili kuonesha kazi zao na hivyo kuonesha umuhimu wa uwakilishi katika Umoja wa Mataifa na mchango wao katika Diplomasia ya Uchumi.
"Hapa New York mna kila sababu ya kujitangaza, nyinyi hapa mnamuingiliano mkubwa, ni nyumbani kwa Umoja wa Mataifa, lazima muoneshe faida ya nyinyi kuwakilishaa nchi kwenye Umoja wa Mataifa, onesheni mchango wenu katika shughuli za diplomasia ya uchumi na mashirika ya kimataifa,"alisema Balozi.
Amewapongeza kwa namna mnavyoshirikiana na Diaspora wa Tanzania walioko jijini New York, na kuawataka waendeleze ushirikiano huo kwani wao ni walezi na wasaidizi wao panapohitajika jambo la kufuatilia
Nimeona mna ushirikiano sana na Diaspora wa hapa, muendelee kuwashirikisha na muendelee kuwa walezi, washauri na msimbague mtu, sisi kama Wizara tunapenda kuwaona mkiwa pamoja, mshirikiane na Idara ya Diaspora katika kutekeleza suala hilo," alisema Balozi Mulamula
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata
Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa jijini New York
Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Ali Suleiman (wa tatu kulia) akizungumza
katika kikao cha Mhe Waziri Mulamul alipokutana na wafanyakazi wa Ofisi
ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New
York
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya
Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...