* DK. Tulia kuongoza harambee CBE Mbeya
Na Mwandishi Wetu
CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimeandaa harambee ya kukusanya Sh bilioni 1.2 kwaajili ya ujenzi wa hosteli za wasichana kwenye kampasi yake jijini Mbeya.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mjema, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee hiyo yenye kauli mbiu “Changia zaidi ya harusi, Uwe sehemu ya kuleta tabasamu kwa watoto wakike’.
Alisema wameamua kuanza na ujenzi wa hosteliza wasichana kutokana na changamoto wanazopata wanapokuw anje ya kampasi kulinganisha na wavulana.
Alisema kilele cha harambee hiyo inayosimamiwa na mlezi wa Kampasi hiyo, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson itakuwa tarehe 24 mwezi huu jijini Mbeya.
Profesa Mjema alisema wanafunzi wengi wa ngazi ya diploma na cheti bado ni wadogo hivyo wanahitaji mazingira mazuri ya kusomea ndani ya kampasi hiyo.
“Siyo kwamba tunawatenga wanafunzi wa kiume bali tunazingatia hali halisi na mazingira yalivyo ndiyo maana tumeamua kuanza na hosteli za wasichana na baadaye tutajenga za wakiume,” alisema Prof Mjema
Aidha, alisema chuo kimefanya jitihada za kuwafikia wadau mbalimbali zikiwemo taasisi na mashirika ya serikali, yasiyo ya serikali na sekta binafsi kuomba michango.
“Tumefikisha ombi letu kwa waheshimiwa wabunge ambao ni wadau muhimu wa maendeleo ya elimu na tunawaomba wadau wote wenye mapenzi mema wastushike mkono ili tukamilishe jambo letu,” alisema
Aliwashukuru wadau mbalimali ambao wameshachangia ujenzi huo na wengine wametoa ahadi zao kufanikisha ujenzi huo.
Aliwataja baadhi yao kuwa ni benki ya NMB, WMA, BRELA, TBS, NHC, St John University, wajumbe wa bodi ya uongozi CBE, wahitimu wa CBE, wanafunzi wasasa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya , Juma Homera ambaye ametoa shilingi 5,000,000.
“Kipekee napenda kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ambaye kiukweli amekuwa ni kiongozi anayejitolea kwa hali na mali kuhakikisha jambo hili linafanikiwa. Mkuruhgenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA naye amekuwa nasi bega kwa bega kukusanya fedha,” alisema
“Kwa niaba ya mlezi wa kampasi ya Mbeya, Dk. Tulia Ackson tunawakaribisha wadau wote wafike kwenye harambee tarehe 24 mwezi huu kwenye hoteli ya Eden jijini Mbeya kuanzia jioni. Tunaomba wadau wote watakaopata ujumbe huu wasikie kilio chetu tujenge hosteli za wasichana,” alisema
Aliwaomba wasamaria wema kuchangia ujenzi huo kupitia akaunti ya NMB 20601100030, TigoPesa 0710 999237 na kupitia akaunti ya MPESA ambayo ni 0742 135979.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee hiyo itakayofanyika Septemba 24 jijini Mbeya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...