Katibu
Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi,
ametoa siku 7 kwa watendaji wa Idara ya Michezo kukamilisha nyaraka za
miradi yote iliyoko chini ya Idara hiyo la sivyo kila mhusika atabeba
mzigo wake.
Dkt. Abbasi ametoa agizo hilo leo hii alipokutana na
watendaji wote wanaosimamia sekta ya michezo nchini kuanzia Idara ya
Maendeleo ya Michezo iliyoko Wizarani, Chuo cha Maendeleo ya Michezo
Malya na Baraza la Michezo (BMT).
“Kuna changamoto kubwa sana za
kiutendaji zilizobainika katika Idara ya Maendeleo ya Michezo kiasi cha
kukwamisha miradi mingi nimekuja kuwaambia hapa nyie ndio wataalamu
sisi tunatafuta hela kuna mabilioni ya fedha Serikali imetenga kila
nyaraka unayouliza kazi zianze unaambiwa bado, kila kitu unachohitaji
ukapewe hela Hazina hakijaandaliwa, sasa tumefanya mabadikiko ya uongozi
wa juu wa Idara hii tunataka sasa kazi na matokeo na sio blah blah
nyingi,” alisema Dkt. Abbasi.
Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara ametoa
siku saba kwa watendaji wanaokaimu katika Idara hiyo kukamilisha
nyaraka hizo ikiwemo miradi ya ujenzi wa viwanja vya kupumzika wananchi,
shule 56 za michezo na ukarabati wa viwanja mbalimbali vya michezo.
“Serikali
inataka kazi na matokeo miradi yote hii mingi ishatengewa fedha na
mingine tunahitajika kupata maandiko yenu wataalamu lakini kwa kiasi
kikubwa imekuwa stori nyingi tu. Sasa baada ya siku 7 hizo kila
atakayekwamisha tutampa jukumu analoonekana analiweza zaidi na si katika
Idara hii muhimu kwa nchi ya maendeleo ya michezo,” alisema.
Wakati
huo huo, Dkt. Abbasi jioni hii amefanya ziara ya kustukiza kwenye
Baraza la Michezo nchini kukagua utekelezaji wa maelekezo ya kulitaka
Baraza hilo kununua vitendea kazi mbalimbali vya kisasa yakiwemo magari
kwa ajili ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...