Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akiwa amebeba mmoja ya watoto Mapacha.

Na Humphrey Shao, Michuzi TV
MKUU wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo leo amekabidhi Pikipiki aina ya Boxer kwa Mwanamama Fatuma ambaye alijifungua watoto wanne kwa wakati mmoja.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo mara baada ya kukabidhi Pikipiki hiyo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate amesema kuwa ameamua kumkabidhi chombo hicho hili kumpunguzia Mama huyo makali ya maisha ya kulea watoto hao.

"Mwaka huu mwezi wa pili alijifungua watoto wanne lakini lengo lake lilikuwa kujifungua mtoto mmoja hivyo baada ya kujifungua tulimpa msaada wa awali wa nepi na nguo lakini sasa lengo la ofisi yangu ni kumpatia kifaa ambacho kitaweza kumsadia kujipatia kipato cha kila siku hili aweze kununua maziwa ya watoto." Amesema DC Jokate.

Ametaja kuwa mara baada ya kujifungua watoto Mama huyo ameweza kusimama shughuli zake zote hivyo awezi kutembea kwenda kujitafutia kipato wala kufanya shughuli yoyote.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ametoa Maelekezo kwa Mtendaji kata wa Mtaa anakotekea Mama huyo kuhakikisha anampatia Dereva ambaye ni Mwaminifu atakayefanya kazi na kumpatia mama huyo pesa ili aweze kusaidika na malezi ya watoto hao.

kwa upande wake Bi Fatuma alimshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuweza kumpatia msaada huo kwani utaweza kumsaidia sana katika kuweza kupata chakula cha watoto hao.

Bi Fatuma ambaye ni Mama wa Watoto Saba alijifungua Mtoto Mmoja katika Uzao wa Kwanza na watoto Mapacha katika uzao wake wa Pili na Katika uzao wake huu wa tatu ameifungua watoto hao wanne kwa wakati mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...