Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe Pallangyo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2022 wakati akizungumzia namna ifakavyofanyika wiki ya Sayasi za Jamii.Mhadhiri wa Idara ya Sosiolojia, Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Egidius Kamanyi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2022. Kulia ni Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe Pallangyo.
Mhadhiri wa Idara ya Sosiolojia na Antrolojia, Ndaki ya Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rechard Sambaiga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2022. Kulia ni Mhadhiri wa Idara ya Sosiolojia, Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Egidius Kamanyi.

NDAKI ya Sayansi za Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, imezindua Wiki ya Sayansi ya Jamii ikiwa ni kuelekea kuhitimisha maadhimisho ya miaka 60 ya chuo hicho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2022 Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe Pallangyo amesema kuwa maadhimisho hayo yataenda sambamba na Wiki ya Sayansi ya Jamii ambapo katika kilele cha maadhimisho watatembelea kituo cha Vijana walioathirika na Uraibu wa dawa za Kulevya (Sober House) iliyopo Kigamboni.

Ameseama Katika Kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Sayansi za Jamii kutakuwa na midahalo itakayoangazia Safari ya Ndaki ya Sayansi za jamii walipotokea, walipo na wanakoelekea.

Katika maadhimisho hayo wanamalengo ya kutoa fursa kwa Ndaki na wadau wake ikiwa pamoja na wanataaluma, wanafunzi, Wahitimu na Waajiri pamoja na jamii nzima kwa kubadilishana uzoefu katika Sayansi za Jamii katika Ujenzi wa Taifa.

Kuonesha Mafanikio ya ndaki ya Sayansi za Jamii iliyoipata tangu kuanzishwa kwakwe miaka 57 iliyoipata hususani katika ufundishaji na kutoa wataalamu mbalimbali waliokatika sekta ya Umma na binafsi.

Amesema kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Mkuu Ofisi ya Rais Menagementi ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dkt. Laurean Ndumbaro

Kauli Mbiu katika maadhimisho hayo ni “Miaka 60 ya Umahili wa Sayansi za Jamii Katika Kufundisha, Utafiti na Huduma za Jamii."

Profesa Pallangyo amesema kuwa Ndaki ya Sayansi za Jamii imekuwa Mstari wa Mbele katika Kutekeleza malengo ya kuanzishwa kwa chuo Kikuu cha Dar Es Salaam hususani katika nyanja mhimu za kuandaa wataalamu wa Sayansi za jamii Kufanya tafiti, kutoa huduma za jamii kupitia hazina ya washauri elekezi waliobobea katika fani zote za Sayansi za Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...