Na Mwandishi wetu - Bungeni

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema,  katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetenga Sh. Bilioni 69.95 kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma katika sekta ya afya ikiwemo uboreshaji wa huduma ya upatikanaji wa dawa, vitenganishi  na vifaa tiba.

Akijibu swali  lililoulizwa na Mhe. Jacqueline Msongozi(Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma)  alipotaka kujua Lini Serikali itaboresha huduma za afya katika vituo  vya afya ili huduma ziendelee kutolewa.

Mhe. Dugange amesema  Serikali inaendelea kuboresha sekta ya afya katika uboreshaji wa huduma za upatikanaji wa dawa kwa kuongeza bajeti ya afya, kuendelea kuajiri watumishi  sekta ya afya na kuwapeleka nchi nzima.

 Pia amesema Serikali itaongeza  bajeti  ya ununuzi wa dawa kwa mwaka wa fedha uliopita na mwaka wa fedha 2022/23 na ununuzi vitenganishi na vifaa tiba.

“Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya nchini kote na vituo vyote vya afya 530 vilivyojengwa vitapatiwa vifaa tiba ili wananchi waweza kupata huduma bora”amesema  Mhe. Dugange.


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...