Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi wa chama cha Mapinduzi, Dr.Edmund Mdolwa ameshiriki ibada ya mazishi ya mtoto wa Mkurugenzi wa kampuni ya Makapo Construction ,Marehemu Deogratius Joseph Peneza aliyefariki dunia tarehe 08.10.2022 na kuzikwa 12.09.2022 katika makaburi ya familia yalioko Mapinga mkoani Pwani.


Akizungumza wakati wa ibada ya kumuaga marehemu  iliyofanyika katika kanisa la KKKT usharika wa Mbezi Beach Baba wa marehemu Mzee Joseph Peneza ambae ni mkurugenzi wa kampuni ya Makapo Construction   Pia ni  Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na Mjumbe kamati ya Siasa Wilaya ya Masasi  alisema ni pigo kwake na familia  kumpoteza kijana mdogo ambaye ndio kwanza alikua anaaza kujitengenezea Maisha yake

Nae mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi wa  CCM Dr. Edmund Mndolwa alisema Kifo ni funzo na ibada lakini hakizoeleki anaitaka familia kuwa na utulivu katika kipindi hiki cha msiba na kuhakikisha wanazidi kumuombea kwa Mungu,kwani wazazi/wazee  wanategemea wakifariki vijana ndio watawazika lakini leo kijana mdogo hana hata mtoto ametangulia

Viongozi mbali mbali wa ccm na wabunge mkoa wa Mtwara walihudhuria Mazishi hayo yaliofanyika Mapinga Bagamoyo na miongoni mwao ni aliyekuwa Mbunge wa Mtwara vijijini Mama Hawa Ghasia na Mbunge wa Ndanda Cecilia Mwambe

Mzee Peneza na mkewe wakiweka shada la maua juu ya kaburi la mtoto wao wakati wa mazishi yaliofanyika Mapinga Bagamoyo Pwani
Mama mfiwa akiingia kanisani wakati wa ibada
Viongoz wa dini wakiweka mchanga juu ya kaburi




 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...