Na Mwandishi Wetu,
HALMASHAURI ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara imevuka lengo kwa kuchanja chanjo ya Polio ya matone watoto 46,137 sawa na asilimia 113.62 wenye umri chini ya miaka mitano katika Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji wa Chanjo ya Polio awamu ya tatu.
Akitoa takwimu hizo Septemba 4,2022 Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Dk.Grace Paul amesema kuwa idadi hiyo imevuka lengo ambalo lilikuwa kuwafikia watoto 40607.
" Kampeni imekamilika salama tumevuka lengo kwa kuchanja watoto wengi zaidi,lengo likikuwa kuwafikia watoto 40607 lakini sisi kwa siku nne tumeweza kuchanja watoto 46137 sawa na asilimia 113.62," amesema Dk. Paul
Amesema takwimu za watoto ambao wamechanja kwa siku tatu mfulululizo zilikuwa zikiongezeka kutokana na wazazi na walezi kuhamasika kuchanja watoto wao chanjo ya Polio ya matone ili kuwakinga na madhara yatokanayo na Ugonjwa wa Polio
Aidha takwimu ya siku ya kwanzawatoto 11,090 sawa na asilimia 109.24 walichanja chanjo ya Polio,siku ya pili watoto waliochanja chanjo ya polio ni 12884 sawa na asilimia 126.9,sikunya tatu watoto waliochanja chanjo ya polio ni 13327 sawa asilimia 131.27 na siku ya nne ambayo ni mwisho wa kampeni watoto waliochanja chanjo ya Polio ni 8836 sawa asilimia 87.03
Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji wa Chanjo ya Polio ya matone kwa Awamu ya Tatu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano(5) ilianza nchi nzima Septemba 1 ,2022 na imemalizika Septemba 4,2022
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...