Bodi
ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)
imewakutanisha wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni
maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba
mwaka 1972.
Akizungumza
leo wakati wa kufungua Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu amesema leo
wamekua na kikao cha wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi
katika ngazi mbalimbali ikiwa na lengo la kuwanoa kwenye mbinu
mbalimbali za mitihani hasa kwenye maeneo yanayokuwa na changamoto kubwa
sana kwa watahiniwa wa Bodi.
Amesema
yapo Masomo yanaleta changamoto Sana na kiwango cha ufahulu unakuwa
mdogo hivyo tumewaletea walimu wa Masomo hayo kutoka vyuo na Taasisi
mbalimbali ili waweze kuwapa uzoefu wao na kuwapa mbinu mbalimbali za
kuweza kujiandaa na mitihani ya Bodi.
"Tumewasisitiza
Sana namna ya kujiandaa wasijiandae kiholelaholela bali waweke muda wa
kutosha kwenye kujifunza kwani kuna tofauti kubwa sana kati ya
watahiniwa wa vyuo na watahiniwa wa mitihani ya Bodi " alisema Temu
Pia
amesema lengo kubwa la NBAA ni kuona wanapandisha kiwango cha ufahulu
kwa mitihani mbalimbali pamoja na kuongeza kiwango cha uelewa ili
kipindi wanapomaliza mitihani yao waweze kuwa wabobezi kwenye masuala ya
Uhasibu na ukaguzi.
Naye
Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo anasema Bodi
hiyo imejipanga vizuri ili kuhakikisha kila mtahiniwa anafanya mitihani
ya Bodi hiyo na kuhakiksiha wanaondoa changamoto zote.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA
Profesa Sylvia Temu akizungumza na watahiniwa
wanaotegemea
kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu
kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972 ambapo kilele chake
ninatarajiwa kufanyika Novemba 28, 2022.
Meneja
wa Idara ya Elimu na Mafunzo, Peter Lyimo akizungumza jambo pamoja na
kumkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu kwa ajili
ya kufungua kikao kazi cha watahiniwa
wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972
Afisa
wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA),
Humphrey Symphorian akizungumza jambo kwenye semina ya watahiniwa
wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50
tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972
Baadhi
wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi, Wakufunzi pamoja na
wafanyakazi wa Bodi wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa
ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia
Temu wakati wakufungua semina kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya
mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa
Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972 iliyofanyika kwenye ofisi za Bodi
hiyo jijini Dar es Salaam.
Semina ikiendelea
Picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...