Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye akizungumza na wageni waalikwa kwenye ukumbi wa Mlimani city kupitia teknolojia ya hologramu, iliyomwezesha kuonekana kama yupe ukumbuni hapo kiuhalisia lakini hakuwepo hapo. Hii ni baada ya Vodacom kuzindua rasmi mtandao wa 5G. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hilda Bujiku.
Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia, Mheshimiwa Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 5G uliofanyika leo Septemba Mosi,2022 jijini Da es Salaam.
Baadhi ya wadau wa teknolojia wakijadili mapinduzi ya kidigitali yanayotarajiwa kuletwa Tanzania na 5G.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hilda Bujiku akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 5G uliofanyika leo Septemba Mosi,2022 jijini Dar es Salaam

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC imezindua huduma ya mpya teknolojia 5G ikisema italeta mapinduzi na kuongeza ushiriki wa Taifa katika kuleta mageuzi ya nne ya viwanda.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Septemba Mosi, 2022 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hilda Bujiku wakati wa halfa ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.

"Teknolojia hii ya 5G inakuja na fursa kubwa hapa nchini kwa wabunifu kuleta bidhaa na huduma mpya kwa wananchi. Vodacom sio tu itaendelea kubuni huduma mpya bali kuwezesha jamii ili kutimiza ndoto za kujenga Taifa bora.

Katika uzinduzi huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliyeeleza kuwa, Mei mwaka huu aliahidi Bungeni kwamba Tanzania itaanzisha 5G hapa nchini jambo hilo limetia leo kwa kampuni ya Vodacom kulitekeleza.

"Tuliposema ilikuwa kama ndoto lakini leo karibu miezi mitatu, lakini Vodacom wametekeleza na kutusaidia kuingia kwenye orodha ya nchi chache Afrika zilizoanzisha huduma ya teknolojia ya 5G.Vodacom wamekuwa wa kwanza kwenye mambo mengi wameanza na M-Pesa na mambo mengine nawashukuru," amesema Nape.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...