Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kigoma
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amepokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa gati la Bandari ya Ujiji ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 38.5.
Kinana amefanya ziara ya kutembelea bandari hiyo leo Septemba 1,2022 baada ya kuwasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.
Akipokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa gati la Bandari ya Ujiji ,Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bandari(TPA) Kanda ya Ziwa ambaye pia anasimamia Bandari ya Kigoma Edward Mabula amesema tayari miundombinu mipya ya maghala ya kuhifadhia shehena ya mizigo , jengo la abiria , ofisi ya walinzi zimekamilika na zinatumika.
Ameongeza na matarajio yao ifikapo novemba 2022 asilimia 61.5 zilizobakia zitakuwa zimekamilika, kukabidhiwa na kuanza kutumika huku akieleza mradi huu unatekelezwa na mkandarasi China Railway 15th group Cooparationi (CR15G) kwa muda wa miezi 24.Ujenzi ulianza Machi 2019 kwa gharama ya Sh.32,525,980,200.00
Akielezea kuhusu bandari hiyo mbele ya Kinana ,Mabula amesema bandari hiyo ni ya tatu kwa ukubwa mkoani Kigoma baada ya Bandari ya Kigoma na Kibirizi.
“Bandari ya Ujiji ni mashuhuri kwa kuhudumia boti za kisasa zenye uwezo wa kubeba hadi tani 30 kwa wakati mmoja ambazo zinabeba bidhaa mbalimbali za biashara na za majumbani kwenda ndani ya nchi jirani za DR Congo na Burundi.Kuhusu utendaji kazi wa bandari hiyo mwaka wa fedha wa 2021/2022 ilihudumia ni tani 1,223 na boti zilikuwa 156.
Akitaja changamoto amesema ni barabara ya kuingia bandari ya Ujiji kutokuwa ya kiwango cha lami ,wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuwa bandari hiyo ni eneo maalum lenye kutakiwa kukidhi viwango vya kimataifa wakati wote.
Wakati mipango ya kuendeleza bandari ya Ujiji amesema moja ni kuitangaza zaidi bandari hiyo ndani na nje ya nchi ili kuongeza wateja wengine watakaopitisha mzigo kwenye bandari.
“TPA kupitia Kituo cha Kigoma kufanya kampeni ya kuwatembelea wateja kwa kushirikiana na TRC kuona namna bora ya kuwahudumia wateja wa ushoroba wa kati kwa gharama nafuu,"amesema Mabula.
Pia kukamilisha mradi wa uboreshaji wa bandari ya Ujiji ili kuanza kuhudumia mzigo kwa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vifaa stahiki vya kisasa kuhudumia mizigo ya aina zote.
Mabula amesema TPA inaendelea kuboresha bandari ya Ujiji ili inufaike na fursa za kuhudumia shehena na mizigo mchanganyiko kwenda ndani ya nchi na kwa majirani zao wa DRC na Burundi.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka sambamba na Viongozi wa Chama na na Serikari Mkoa huo wakitembelea bandari hiyo leo Septemba 1,2022 baada ya kuwasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja. PICHA NA MICHUZI JR-KIGOMA
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman akimueleza jambo Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Kanda ya Ziwa ambaye pia anasimamia Bandari ya Kigoma Edward Mabula alipofanya ziara ya kutembelea bandari hiyo leo Septemba 1,2022 baada ya kuwasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman akimsikiliza Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bandari (TPA) Kanda ya Ziwa ambaye pia anasimamia Bandari ya Kigoma Edward Mabula alipofanya ziara ya kutembelea bandari hiyo leo Septemba 1,2022 baada ya kuwasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.PICHA NA MICHUZI JR-KIGOMA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...