
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana,Akiwa amenyenyua juu kitabu Cha Historia ya Moka wa Kigoma mara baada ya Kukabidhiwa rasmi na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kigoma.
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
MAKAMU Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman
Kinana, amesema Chama hakitamvumilia mwanachama yeyote ambaye anataka
kuwania nafasi ya uongozi kwa kutumia udini, ukabila na ukanda.
Amesisitiza
Chama kinawatafuta watu wa namna hiyo na endapo kitaelezwa kuna mtu
anashughulika na ukabila, udini na ukanda jina lake litakuwa la kwanza
kuondolewa katika orodha ya wanaowania nafasi za uongozi ndani ya CCM.
Kinana
ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa
Kigoma ambapo akiwa katika kikao hicho amepokea taarifa ya uwepo wa
baadhi ya wana CCM wanaotumia dini na ukabila hususan katika kipindi
hiki cha uchaguzi wa ndani wa Chama kushawishi wapigakura.
“Mtu
wa kwanza kupunguzwa ni yule ambaye unaambiwa anahangaika na ukabila
huyu kata na mwondoe katika orodha, huyu anashughulika na ukabila
tunasema mwondoe kwenye orodha. Huyu ana mhukumu mtu kwa dini
tunawaambia muondoe kwenye orodha.
“Jambo moja niliseme ambalo
lipo katika taarifa ya Katibu wa CCM wa Mkoa (Mobutu Malima) kwamba
unapofika wakati wa uchaguzi, Kamati ya Siasa imeonesha ujasiri wa
kuandika kuna tatizo la ukabila, ukanda na udini.
“Ukiona
kiongozi anahangaika na ukabila, kwa maoni yangu mimi hufai hata
kupigiwa kura kwa sababu kila mtu ana sifa zake, tumpime mtu kwa sifa,
si kwa kabila, sijui kama mnakumbuka hotuba ya Baba wa Taifa ya ukabila,
kwamba tunakwenda karne ya 21 ukiwa umepanda basi la ukabila.
“Na
hili lilimuudhi sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, wako wakuu wa
Wilaya wametoka mikoa mingine kabisa, wako watu ambao wameishi hapa
(Kigoma) na Watanzania wenzao, watu wanawajua, wanawaheshimu,
wanawathamini.
“Wanagombea, wana sifa, wanafaa, wana msaada
halafu unamhukumu kwa kitu kimoja tu, kabila lake, kweli sawa hii? Ni
kiongozi aliyefilisika nataka niwaambie haya mambo sio ya wanachama bali
yanatengenezwa na viongozi,” alisema.
Alifafanua kuwa kiongozi anaona mambo yake hayaendi vizuri na fursa ya kuchaguliwa haipo, anahamia kwenye hoja za ubaguzi.
“Wanachama hawana hizo sifa, mtu achaguweli kwa sifa zake, mtu achaguliwe na apimwe kwa uwezo wake.
“Mtu
apimwe kwa historia yake ya utendaji lakini usifike mahali ukasema huyu
kabila langu, kabila lako hovyo, kabila lako uvivu, kabila hana uwezo,
kabila lako hafai, hajui hata anachokiomba.
“Lakini unasema
kabila langu, oooh tunatoka eneo moja, haya ukishamchagua mnayetoka eneo
moja anakusaidia nini? Hakuna, hana mawazo, hana jambo jipya, hana la
kukwambia. Nyie ni mashahidi nchi yetu hii imeongozwa na watu waliotoka
kwenye makabila madogo.
“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kabila
lake ukihesabu wako wangapi, sijui hata kama walikuwa wanafika 100,000
lakini aliongoza nchi hii miaka 24, mpaka leo hatujamsahau Mwalimu kwa
uongozi bora, hatumhukumu kwa kabila lake , hapana, tuna mhukumu kwa
uwezo.
“Hivyo hivyo Mzee Ali Hassan Mwinyi anatoka kwenye eneo
dogo, mzee Mkapa ametoka eneo dogo lakini amefanya kazi kubwa nzuri ,
sasa tukikaa watu tunawahukumu kwa ukabila na ukiona mtu anahangaika na
ukabila tafadhali mkateni jina lake, achenani naye,”alisema Kinana.
Alisisitiza
kwamba CCM inawatafuta hao watu wa namna hiyo na kwamba wakiambiwa kuna
mtu anashughulika na ukabila, udini na ukanda hataachwa na bahati nzuri
hiyo habari ikaja kwetu(CCM) , maana yake kazi kubwa waliyonayo mwaka
huu ,watu waliojitokez kugombea nafasi za uongozi ni wengi na wenye sifa
zote.
“Kwa hiyo hatuna ufuraka wa watu waliogombea , kazi kubwa
tulinayo ni kupunguza watu. Mtu wa kwanza kupunguzwa ni yule ambaye
unaambiwa anahangaika na ukabila, udini na ukabila.Mtu huyo tunaondoa
jina lake kwenye orodha ya wagombea,”alisema Kinana.
Aliongeza
Mwalimu Nyerere alikuwa anasema hatutafuti askofu, hatutafuti sheikh
wala au Imamu wa Msikiti, bali wanatafuta kiongozi wa kuongoza
wanzake.“Sasa ndugu zangu viongozi ninyi ndio mko hapa , Chama hiki Mkoa
wa Kigoma ni ninyi.Ninyi ndio mnaotengeneza muelekeo wa Chama chetu,
ndio mnaomua nani awe nani,
“Ninyi ndio mnaotengeneza uhai wa
hiki Chama, mnaaamua Chama hiki kiwe na uhai au kisiwe, lakini kama uhai
wa chama , maendeleo ya mkoa huu msingi wake utakuwa dini ya mtu
itakuwa tatizo kubwa sana, niwaombe ndugu zangu msihangaike na hili
jambo, angalieni uwezo wa mtu hata kama ni ndugu yako,
“Hata kama
ni ndugu mmezaliwa naye na hana uwezo mwambie tu we ni ndugu yangu
lakini kwa bahati mbaya uwezo huna .Mtu anakuleta meseji ananiambia
Makamu Mwenyekiti naomba nije ni kuone, naamuliza kuna shida gani, ooo
nina jambo langu, niambie kwenye simu , aah ni vizuri tukaonana.
“Basi
mimi najua hiyo kuonana ina maana yeke , basi namwambia njoo saa fulani
kama nyumbani au ofisini akija anakwambia nagombea .Unagombea nafasi
gani?Nagombea nafasi fulani , halafu unamuuliza maswali ya msingi, si
muulizi kabila, simuulizi dini yake bali namuuliza maswali ya
msingi,”alisema Kinana.
Alisema anamuuliza huko kwenye mkoa
unaotaka kugombea wewe Wilaya ziko ngapi?Anakwambia anadhani kama.“Sasa
kama unaanza na nadhani hata fuhai kugombea na kushauri achana na
kuombea.Unamuuliza majimbo ya wabunge yako mangapi, hajui na anataka
kugombea.
“Lakini ndio hao wakirudi msingi wa kutafuta uongozi
sio uwezo ,sio sifa bali anachoona kwake atarudi na atazungumza na jamaa
zake ili wamsadie.Na mimi namwambia mtu ukweli , namuuliza maswali ya
msingi, swali la kwanza, la pili la tatu akishindwa nawambia usipoteze
muda wako , usijipe presha isiyo na sababu
“Unataka ushauri mzuri
kwangu achana na hili jambo si lako huliwezi , sasa ananiambia baada ya
hilo unanishauri nini?Namwambia ndio nimeshakushauri achana nalo.Hakuna
ushauri mwingine zaidi ya hapo , kwa hiyo wako watu wengi sana wana
uwezo , wanafaa na wengine wana uwezo mzuri , mabingwa, watu waadilifu,
mahodari , lakini kila akitazama maneno yanayosemwa na udini udini,
ukabila anaamua kulaa mbali.
“Hapa hapanifai , nikitaka kugombea
nitaambiwa mimi sio kabila lako, kwa hiyo tunawakosa watu wazuri
kwasababu ameona wale wapiga kura wameweka vigezo vya hovyo na wapiga
kura wameweka vigezo vya hovyo kwasababu wanaowangoza ndio wamewakea
hivyo vigezo , ndugu zangu hii nchi imeongozwa vizuri na viongozi.
“Baba
wa taifa mwalimu Nyerere, aliwahi kusema karne hii ya 21 si karne ya
udini , nadhani si karne ya ukabila , wala ukanda , wala eneo .Mimi
nawajua wanachama wengi watanzania wala hili jambo halimo kichwani mwao ,
wanaopandikiza kwenye vichwa vyao ni mgombea, anataka kugombea unaona
kura hazitoshi anaenda kwenye ukabila.
“Na watu wanakwenda kwenye
ukabila ni pale anapoona kabila lake wapiga kura wake ni wengi
,anahamia pale kwenye ukabila, kwa hiyo badala ya kutafuta hisia au
uwezo wa mtu anatafuta mioyo ya watu kuonewa huruma , kwa hiyo nataka
niwasihi ninyi ndio viongozi tunawategemea , Makao Makuu ya Chama pale
hatujui watu, ninyi ndio mnaowafahamu watu wote.
“Na ni vizuri
ukiona mtu anaendesha jambo kama hilo usimseme pembeni , unamuita,
kamati ya siasa ya mkoa inakaa inamuita .Leo nimeletewa meseji kuna mtu
mmoja wa halmashauri fulani analeta vurugu msipate naye tabu.
“Mnauliza
anafanya nini , anasema yeye kuna watu hataki mtu fulani achukue
uongozi , sasa wewe Mwenyekiti si una kura moja kwanini unawanyima
wenzako nafasi, anatumia ule uenyekiti wa halmashauri , nikawaambia
jambo lake rahisi mleteni kwenye Kamati ya maadili , tumjadili,
tutamshughulikia, basi.
“Hakuna namna nyingine, na Chama hiki
kina kanuni, Katiba, kina maadili , kanuni za uongozi na kanuni za
utumishi, zote zimeandikwa na kila kitu kimeandikwa vizuri wala hatutoi
nje ya utaratibu , na kwenye maadili adhabu imeandikwa humo ndani, kila
kitu kipo hatuzui mambo.''
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania
Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na viongozi wa
Chama na serikali pamoja na Wanachama wa CCM katika Mkutano wa ndani
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Anglikana Mkoa wa Kigoma akiwa katika ziara
ya kikazi kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya
CCM 2020-2025. Katika ziara hiyo Kinana ameambatana na Katibu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu
Shaka.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kigoma kwa ziara ya kikazi kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025. Katika ziara hiyo Kinana ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Mwenyekiti MSTAAFU wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Kassim Nyamkunga baada ya kuwasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025. Katika ziara hiyo Kinana ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana,Akizungumza na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania
Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiwa ameambatana na viongozi
wengine akikagua ujenzi wa bandari ya Ujiji mkoani Kigoma akiwa katika
ziara ya kikazi kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM 2020-2025. Katika ziara hiyo Kinana ameambatana na
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi,
Shaka Hamdu Shaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...