Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, kesho anatarajiwa kuwaongoza wahandisi katika maadhimisho ya siku ya wahandisi hapa nchini.
Akizungumza jijini Dodoma leo Msajili wa Bodi ya Wahandisi (ERB), Eng. Benard Kavishe, amesema maandalizi kwa ajili ya maadhimisho hayo yamekamilika ambapo takriban wahandisi 3500 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki.
Eng. Kavishe amesema kuwa maadhimisho hayo yatawawezesha wahandisi kuuonesha umma nini wahandisi wa Tanzania wanaweza kufanya katika kuleta maendeleo ya nchi na kukuza uchumi, kuwawezesha wahandisi kuonesho ubunifu wa teknolojia mpya zinazotumiwa na wahandisi, kuwatambua na kuwapongeza wahandisi wanaofanya vizuri katika kazi zao na kuwapongeza wanafunzi toka vyuo vikuu waliofanya vizuri katika kozi za uhandisi.
Aidha Eng. Kavishe amesema takriban wahandisi 400 watakula kiapo cha utii na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia taaluma na hivyo kuuwezesha umma kujenga imani kwa wahandisi na kuthamini kazi za kihandisi.
Maadhimisho ya siku ya wahandisi mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu na Uendelezaji wa Ujuzi katika Kuimarisha Maendeleo Endelevu ya Uchumi wa Taifa: mtazamo wa kihandisi”.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo Eng. Benedict Mukama, amesema wahandisi kutoka nchi za Kenya, Uganda na Zambia wameshawasili nchini kuungana na wahandisi wa Tanzania na wengine watashiriki kupitia mitandao ili kuwezesha maadhimisho hayo kufuatiliwa duniani kote.
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Benard Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania yatakayofanyika Septemba 22 na 23 2022, Jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...