Baadhi ya maafisa Habari wakiwa katika majadiliano kuhusiana na kile walichojifunza.
Baadhi ya maafisa habari wakifuatilia mafunzo yanayotolewa.
Na Devota Mwachang'a, Mwanza
MAAFISA habari wa Halmashauri nchini wameshauriwa kutumia mitandao ya kijamii kuandika na kusambaza taarifa zenye tija za maendeleo ikiwemo miradi ya kuimarisha utekelezaji wa elimu bora nchini.
Ushauri huo umetolea na Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) toka TAMISEMI Godfrey Isinika akielezea umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii kwa wadau wa Habari nchini kusambaza taarifa sahihi na zenye tija kwa sekta ya elimu.
"Yatumieni makundi yenu ya mitandao ya kijamii (social media) kutuma link zinazoambatana na taarifa fupi itakayowezesha wasomaji kutembelea moja kwa moja kwenye kurasa za taasisi badala ya kutuma picha tu," amesema Isinika.
Maafisa Habari toka mikoa ya Mara, Simiyu na Singida wanakutana Mwanza katika mafunzo ya Siku tatu yaliyoandaliwa na Shirika na Cambridge Education Tanzania kupitia Mradi wa serikali wa Shule Bora unaofadhiriwa na Shirika la maendeleo la Uingereza( UKaid). Mafunzo haya nimoja wapo ya mikakati ya kuimarisha ukusanyaji wa taarifa, uandishi na usambazaji wa habari za elimu bora katika mikoa tisa ya tanzania ikiwemo Mara, Simiyu, Kigoma, Pwani, Singida, Dodoma, Tanga, Katavi na Rukwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...