*Asema Serikali ya Awamu ya Sita inaandika historia kukamilika kabla ya muda uliopangwa
* Asema ujenzi daraja la Wami linawaumbua waliokuwa wanabeza , Rais anaupiga mwingi
Na Said Mwishehe,Pwani
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Chama hicho kinaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati inavyoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Shaka aliyasema hayo leo Septamba 18,222 baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na fedha zaidi ya Sh.bilioni 75 zimepangwa kutumika hadi kukamilika kwa daraja hilo ambalo linakwenda kuandika historia ya kuwa mradi wa kwanza nchini kukamilika kabla ya muda uliopangwa na wakandarasi.
"Wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani kulikuwa na maneno mengi kuhusu daraja hili la Wami na si hili tu bali maneno yalikuwa mengi Rais Samia hataendeleza mirad hii ya kimkakati,j wiki mbili zilizopita tulikuwa Mwanza tumeona ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria.
"Tumeona ujenzi wa meli MV.Mwanza unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria na leo niko hapa daraja la Wami nashuhudia kwa macho yangu, mikono yangu lakini ukisimama hapa ukiangalia kule mbele unaona namna gani ambavyo Pwani na Tanga inavyong'ara kupitia daraja hili
"Wakati Rais Samia anapokea kijiti cha uongozi daraja hili kwa miaka mitatu lilijengwa kwa asilimia 47 tu tena kwa miaka mitatu. Leo hii ndani ya miezi 18 Rais Samia amesimamia ujenzi wa daraja hili limejengwa kwa asilimia 42.2 ndani ya miezi 18 , na fedha zote zimetoka kwa wakati kwasababu fedha isingetoka kwa wakati leo wakandarasi wasingetuonesha kazi kubwa kama hii ambayo imefanyika," amesema Shaka.
Ameongeza kwamba na fedha zote zimetoka kwa wakati na hivyo ukichukua asilimia 47 na asilimia 42.2 unapata asilimia 89.2 kati ya hizo kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa ya Rais Samia Suluhu Hassan huku akieleza kwamba hapo ndipo unaona namna gani ambavyo Watanzania wananufaika na kodi zao kwasababu fedha iliyotoka kwenye daraja hililo ni fedha yetu ya ndani.
"Hakuna fedha ya mjomba ,hakuna fedha ya msaada ,ni fedha ya watoka jasho wa Tanzania ndio imefanya kazi hii na mtaalam alikuwa ananiambia katika historia ya nchi yetu na mimi nimefuatilia iko hivyo , hili litakuwa daraja la kwanza kukamilika kabla ya wakati uliokadiriwa ,daraja hili lilikadiriwa litumie miaka minne lakini tutalifungua kabla ya Novemba.
"Pengine na kungekuwa na muda wa ziada lakini wanakimbizana usiku na mchana kuhakikisha kwamba ndani ya mwisho wa mwezi huu wa Septemba daraja hili linaanza kazi. Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi nzuri sana na wakati mwingine tusiache uongo uelee mbele ya ukweli lazima tuwe na uthubutu,lazima tuwe na utayari wa kuzungumza yale mazuri na mema yanayofanywa kwa ajili ya maslahi ya Watanzania ndani ya nchi yetu.
"Leo hii tunakwenda kusahau shida , tunakwenda kusahau adha , tunakwenda kusahau vilio , kukamilika kwa daraja hili na tunafanya ukarabati wa daraja la zamani,ina maana kwamba kwa dharura yoyote ile ikitokea hapa tunao uwezo wa kutumia daraja letu lile ambalo tuliozea kutumia.Niwashukuru wabunge kwa kuisimamia vema Serikali,lakini Mkuu wa Mkoa nikushukuru sana wewe na timu yako ,wakuu wa Wilaya...
"Wakurugenzi kwa namna ambavyo mnatafsiri kwa vitendo dhana na azma ya Rais Samia Suluhu Hassan kushusha maendeleo chini kabisa ,nimekusikiliza vizuri sana ,mmetajamabilioni ya shilingi yaliyotumika kwenye miradi ya maendeleo,Mmezungunza fedha nyingi za walipa kodi na namna ambavyo zimetapakaa kwenye miradi ya maendeleo,"alisema Shaka.
Amefafanua katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu kwenye Ibara ya 55 kifungu D ,kifungu kidogo cha kwanza,ndani ya miaka mitano wameabisha madaraja yatakayojengwa ,lakini hawatajenga madaraja tu bali wataimarisha na huduma zote za kijamii, kiuchumi hata kisiasa ndani ya nchi yetu.
"Rais Samia amedhamiria na mimi nataka niwaambie katika Rais ambaye hatutafanya kazi ya kampeni 2025 ni Rais Samia Suluhu Hassan,kila Mtanzania mwenye akili yake ,kila Mtanzania mwenye maarifa yake ,kila Mtanzania mwenye kuona anaona namna ambavyo fursa zinavyofunguka ndani ya nchi yetu,miradi ya maendeleo inaendelea, fursa za kiuchumi zinakuja ,mahusiano yetu yanafunguka lakini uhusiano wetu baina ya Mkoa na mkoa, wilaya na Wilaya .
"Urafiki na udugu unakuwa siku hadi siku ili kurasimisha na kuharakisha maendeleo ya haraka ,Rais Samia amekuwa na uongozi shirikishi ,Rais Samia amekuwa na uongozi funganishi lakini viongozi karibia asilimia 90 walioteuliwa,"amesema.
Ameongeza wateule wa Rais Samia wanafanya kazi nzuri sana lazima nao w huku akiwaomba Watanzania waendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Serikali."Tutoe ushirikiano kwa Rais wetu, dhamira ya Rais Samia ni nzuri, wale wachache wanayoyafikiria sisi hatupo huko, nia ni moja tu kuongeza Tanzania.
"Chama chetu tulichukua ahadi kwa Watanzania , hivyo hawatajutia uamuzi wao wa kukiamini Chama Cha Mapinduzi 2020/2025, bahati nzuri sisi sasa hivi hatuangalii nani atakukuwa Rais kwasababu mgombea urais yupo Samia Suluhu Hassan.
"Sasa hivi tunakimbizana na maendeleo ya Watanzania ,ndio kazi tuliyokuwa nayo ,tusipoteze muda.Chama hiki kwenye mambo ya msingi huwa tunaambizana ukweli ,hatuhangaiki na mgombea urais maana tunaye, tunasubiri muda tu na kwa kazi anayofanya unadhani nani atamnyima kura Rais Samia,hayupo,"ameeleza Shaka.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani,Mhandisi Baraka Mwambage kuhusu Daraja la Wami alipotembelea ujenzi wa daraja hilo leo Septemba 18,2022 mkoani Pwani,pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge.
Katibu Wa Itikadi Na Uenezi CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka ,Wananchi na Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakipita katika Njia ya Watembea kwa miguu Kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akiwa na viongozi, wana CCM na wataalamu akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage kuhusu Daraja la Wami mkoani humo alipotembelea ujenzi wa daraja hilo leo Septemba 2022 mkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...