Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii zimeanza kutekeleza maelekezo ya Mawaziri Mhe. Mohamed Mchengerwa pamoja na Mhe. Dkt. Pindi Chana ya kubainisha maeneo na mkakati wa ushirikiano katika Sekta za Utamaduni, Sanaa, Michezo pamoja na Utalii waliyoyatoa Septemba 16, 2022, jijini Dodoma.

Kikao hicho cha ngazi ya wataalamu kutoka Wizara hizo kinafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Septemba 26-28, 2022 katika Ofisi za Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo zilizopo Mtumba Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Aidha, maelekezo hayo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kwa Wizara hizo ambapo alizitaka kukaa pamoja na kundaa mkakati wa pamoja wa kutumia matamasha kukuza Utalii nchini.




Wajumbe kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika kikao cha siku tatu kuanzia Septemba 26-28, 2022 kutekeleza maelekezo ya Mawaziri Mhe. Mohamed Mchengerwa pamoja na Mhe. Dkt. Pindi Chana waliyoyatoa Septemba 16, 2022, jijini Dodoma kuandaa mkakati na kubainisha maeneo ya ushirikiano katika sekta za Utamaduni, Sanaa, Michezo hatua itakayosaidia kukuza Utalii nchini.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...