Njombe
Mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati 25 - 28 amekutwa ameuawa katika msitu wa miti uliopo kwenye eneo la Muungano katika kijiji cha Kifanya halmashauri ya mji wa Njombe akiwa na jeraha kubwa eneo la shingoni na michubuko sehemu za usoni.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema mwili huo umepatikana Septemba tatu mara baada ya watoto kutoa taarifa walipoona mwili huo,lakini hata hivyo mwanamke huyo hajatambulika kuwa ni mkazi wa wapi na tayari jeshi la polisi linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.
“Mtu huyu ameuawa na baada ya kuwatangazia wananchi hajatambulika,amepoteza maisha akiwa amevaa dela la rangi ya bluu lenye michirizi ya Njano akiwa amesuka rasta”amesema Kamanda Issah
Aidha kamanda Issah ametoa wito kwa wananchi wa maeneo ya karibu kama kuna mtu amepotea katika maeneo yao akiwa amevaa mavazi ya aina hiyo aweze kufika katika hospitali ya mji wa Njombe Kibena sehemu ulipohifadhiwa mwili huo kwa ajili ya kuutambua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...