Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi wa chama cha Mapinduzi Edmund Mdolwa ameshiriki ibada ya mazishi ya mtoto wa Mkurugenzi wa kampuni ya Makapo Construction ,Godfrey Joseph Peneza aliyefariki dunia tarehe 8,09,2022 .
Akizungumza wakati wa ibada ya kumuaga marehemu iliyofanyika katika kanisa la KKKT usharika wa Mbez Beach Baba wa marehemu mzee ,Joseph Peneza alisema ni pigo kwake na familia kumpoteza kijana mdogo ambaye ndio kwanza alikua anaaza kujitengenezea Maisha yake
Nae mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi wa Ccm Edmund Mndolwa alisema Kifo ni funzo na ibada lakini hakizoeleki anaitaka familia kuwa na utulivu katika kipindi hiki cha msiba na kuhakikisha wanazidi kumuombea kwa mungu kwan wazazi wanategemea wazee wakifariki vijana ndio watawazika lakini leo kijana mdogo hana hata mtoto ametangulia
Viongozi mbali mbali wa ccm na wabunge mkoa wa Mtwara walihudhuria Mazishi hayo yaliofanyika Mapinga Bagamoyo na miongoni mwao ni Mbunge wa Mtwara vijijini Mama Hawa Ghasia na Mbunge wa Ndanda Cecilia Mwambe.


Mzee Joseph Peneza na mkewe wakitoa heshima ya mwisho katika jeneza la mtoto wao


Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi CCM,Edmund Mndolwa akiaga wakati wa mazishi yaliofanyika Mapinga Bagamoyo


.jpeg)


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...