Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Arusha


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) inatarajia kutoa huduma ya maji kwa zaidi ya asilimia 95 ifikapo 2025.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Mhandisi Justine Rujomba wakati akitoa taarifa fupi za utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na AUWSA.

“Tumejipanga mpaka mwaka 2025 Arusha tutakuwa tumevuka lengo la Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na tutakuwa tunatoa huduma ya maji kwa zaidi ya asilimia 95 katika jiji la Arusha” amefafanua, Mhandisi Rujomba.

Ameongeza kuwa, matokeo ya asilimia hizo yametokana na ongezeko la maji katika mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira unaotekelezwa jijini humo ambapo mpaka sasa wamepata jumla ya lita milioni 200 wakati mahitaji ni milioni 109.

Aidha, ameeleza kuwa, mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira wa jijini Arusha ni mradi wa pili kwa ukubwa Tanzania ambao unakadiriwa kutekelezwa kwa jumla ya Shilingi za Kitanzania billion 520, mradi wa kwanza ni mradi wa maji wa Ziwa Victoria ambao unatekelezwa kwa thamani ya Shilingi bilioni 600.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) inatekeleza mradi mkubwa wa maji kwa lengo la kuondoa kero ya upungufu wa majisafi na uondoaji majitaka katika Jiji hilo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...