Benki ya NCBA imewazawadia pikipiki washindi watatu wa kampeni ya Mpawa ijulikanayo kwa jina la Chuzi Limekubali kwa mara ya pili mfululizo katika tukio lililotokea katika viwanja vya Zakhem Mbagala. Kampeni hiyo ilianza Agosti mwaka huu.

Kampeni hiyo inafanyika kwa ushirikiano na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, ambayo inawahimiza wateja kuweka akiba, kukopa na kurejesha mikopo ili kujishindia zawadi kila siku na kila wiki.

Fulgence Otaru, mfanyabiashara kutoka Dar es Salaam, alielezea furaha yake baada ya kushinda pikipiki. "Ilikuwa vigumu kwangu kuamini mwanzoni, lakini baada ya simu kadhaa kutoka kwa kitengo chao cha huduma kwa wateja, mashaka yangu yaliondolewa. Nataka kuhimiza kila mtu aanze kuweka akiba na Mpawa mara moja kwa sababu mikopo ni ya haraka na rahisi.' Alisema.

Naye Richard Mkoba, mkulima kutoka Pwani na mshindi wa pikipiki, alipongeza kampeni hio baada ya kukiri kuwa zawadi hiyo itainua shughuli zake za kilimo. "Nyinyi (NCBA) mmekuwa benki ya watu - pikipiki hii ina maana kubwa kwa safari zangu za kwenda na kurudi shambani," anasema. Siamini nilishinda pikipiki baada ya siku tatu tu za ushiriki. Asanteni sana.’’

Afisa wa huduma kwa wateja wa NCBA, Maria Mabella, alibainisha kuwa Mpawa imekuwa kipengele muhimu kwa wateja kwani inainua matarajio ya Watanzania kupata mikopo ya haraka yenye riba nafuu sana.

Mabella alinukuliwa akisema, "Kwa upande mkubwa, kampeni hii inalenga kuwahamasisha wateja wetu nchi nzima na Watanzania kwa ujumla kuanza na kuendeleza tabia ya kuweka akiba ya fedha zao kupitia Mpawa. Halikadhalika, fursa hii inasimama ili kuwapa manufaa mengi zaidi ikiwa ni pamoja na kupata mikopo ya haraka na kwa riba nafuu kuliko sehemu au huduma nyingine yoyote."

Tanzania ni mojawapo ya soko la kimataifa la ushindani na linalokuwa kwa kasi la huduma za fedha kwa njia ya simu. Katika hali hiyo, kampeni hio inatoa motisha kwa wateja kwani wana nafasi ya kujishindia pikipiki mpya kila wanaporejesha mikopo kwa wakati na kuweka fedha zao Mpawa.

Mabella alidokeza kuwa "wateja wana nafasi ya kujishindia hadi Sh 50,000 pesa taslimu wanaporejesha mikopo yao ndani ya siku sita. Kila wiki tangu wiki iliyopita, tumewazawadia wateja zaidi ya hamsini waliolipa mikopo yao mapema na kuweka akiba."

Kila mwezi, wateja wanaoweka akiba nasi katika kipindi hiki cha kampeni watakuwa na nafasi ya kujishindia mara mbili ya akiba yao kuanzia shilingi elfu kumi na zawadi kubwa kuliko zote itakuwa kitita cha shilingi milioni tano mwishoni mwa kampeni’’. aliongeza.

Kwa miaka mingi, huduma ya Mpawa imewanufaisha wateja wasiopungua milioni 6 kote Tanzania ambao kwa sasa wananufaika na mikopo midogomidogo isiyo na kikomo cha hadi shilingi laki tano.



Meneja Masoko kutoka Benki ya NCBA, Solomon Kawiche (wa kwanza kushoto), akiwazawadia pikipiki washindi wa awamu ya pili wa kampeni ya Mpawa iliyopewa jina la “Chuzi Limekubali” kwa kushirikiana na Vodacom kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala. Wa pili kushoto ni Fulgence Otaru, mshindi kutoka Dar es Salaam; wa tatu kushoto ni Maria Mabella, afisa huduma kwa wateja kutoka Benki ya NCBA; na kulia kabisa ni Richard Mkoba, mshindi kutoka mkoani Pwani.

Afisa huduma kwa wateja kutoka Benki ya NCBA Maria Mabella (wa kwanza kulia) akimkabidhi pikipiki Richard Mkoba (katikati) kutoka Pwani, mmoja wa washindi wa awamu ya pili wa kampeni ya Mpawa iliyopewa jina la Chuzi Limekubali kwa kushirikiana na Vodacom. Upande wa kwanza kulia ni Fulgence Otaru, mshindi mwingine wa kampeni kutoka Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Zakhem huko Mbagala Septemba 23.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...