Na Mwandishi Wetu, Mara
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani Mara, kuhakikisha wanawasaka watuhumiwa waliohusika na mauaji ya Mzee Omary Iyombe Mkazi wa Kijiji cha Kizaru, Kata ya Muriaza, Wilayani Butiama na kuwaomba wananchi wa Kata hiyo kuwa wavumilivu wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi.
Akizungumza na Wananchi wa Kata hiyo, jana, Sagini amesema Serikali haiwezi ikachezewa lazima watuhumiwa wakamatwe haraka iwezekanavyo na wachukuliwe hatua kali.
"Wananchi wa Kijiji hiki na Kata hii kwa ujumla msijihusishe na vitendo vya mauaji kwani Serikali kupitia Jeshi la Polisi wako macho na watawachukulia hatua kali wale wote watakaojihusisha na vitendo hivyo," alisema Sagini.
Aidha, Naibu Waziri Sagini alishiriki mazishi ya marehemu huyo Omary Iyombe ambaye ni Mkazi wa Kitongoji cha Kwigina katika Kata hiyo, Wilayani Butiama aliyeuwawa na watu wasiojulikana kwa kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na Wananchi wa Kata ya Muriaza, Wilayani Butiama, Mkoani Mara, jana, ambapo amelaigiza Jeshi la Polisi Mkoani humo, kuhakikisha wanawasaka watuhumiwa waliohusika na mauaji ya Mzee Omary Iyombe Mkazi wa Kijiji cha Kizaru Wilayani humo, na amewaomba wananchi wa Kata hiyo kuwa wavumilivu wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...