RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, kilichotokea tarehe 08 Septemba, 2022 nchini Uskochi

Maombolezo hayo yataanza tarehe 10 Septemba, 2022 hadi tarehe !4 Septemba, 2022.

Katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye balozi zetu pia.

Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa kiongozi wao nchini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...