RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Ripoti ya Sisi ni Wamoja, Mtazamo wa Wananchi Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa, utafiti uliofanywa na Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar, akikabidhiwa na Ndg.Rashid Azizi Rashid (kulia kwake) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) Bi. Salma Haji Saadat, baada ya kumaliza mazungumzo na Uongozi wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI) yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi Nchini Tanzania Bi. Sandy Quimbaya (kulia kwa Rais) ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika leo 1-9-2022 katika ukumbi wa Ikulu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI) Bi. Sandy Quimbaya, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...