Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakati akiagana na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama alipokuwa akiondoka leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuelekea Jijini Dar es Salaam ambapo kesho atahudhuria katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM,kitakachofanyika ukumbi wa Ofisi ya CCM Lumumba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi alipokuwa akisalimiana na Viongozi akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makala (katikati) wakati wa mapokezi yake mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Jijini Dar es Salaam leo, akihudhuria katika Kikao cha Kamati Kuu kitachofanyika kesho katika Ofisi ya CCM Lumumba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akiagana na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Hemedi Suleiman leo alipoondoka kuelekea Jijini Dar es Salaam ambapo atahudhuria katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM,kitakachofanyika kesho katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Lumumba.[Picha na Ikulu.] 06 sept 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...