IMEELEZWA kuwa vivu kupita kiasi kwa wanandoa na wapenzi ,hali hiyo
uchangia watu kupata tatizo la afya ya akili na kusababisha kufanya matukio ya kikatili.

Hayo yalisemwa na mkurungenzi wa mahusiano Mayasa Kalinga kutoka Jukwaa la kupambana  kuzuia tabia za watu kujinyonga Tanzania (TSPC).


Mayasa ambaye alitoa mada kwa washiriki wa semina za Jinsia na Maendeleo ( GDSS),mada iliyokuwa ikihusu,afya ya akili na wimbi la ukatili kwa wanandoa na wapenzi,alisema kuwa matukio ya kikatili yanaendelea kuwa wingi hapa nchini.

"Wivu kupita kiasi kwa wanandoa na wapenzi,husababisha  watu kupata ugonjwa wa afya ya akili," alisema.

Aliongeza kuwa unyanyasaji ubaguzi na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wanawake,vimekuwa kichocheo katika kudorolesha afya ya akili kwa kwa wanawake.

Alisema takwimu za jeshi la polisi kuanzia Januari mwaka jana hadi mwezi Juni 2021 watu 15,131 walifanyiwa ukatili wa kijinsia .

" Kuhusu ripoti hiyo,ilionyesha ongezeko mauaji kwa wanawake walio katika ndoa," alisema.

Aliongeza kuwa matukio ya mauaji na ukatili wa kijinsia hasa kwa wanandoa yameendelea kuongezeka nchini Tanzania,hali iliyoibua sintofahamu kuhusu usalama wa hali ya Afya ya akili na usimamizi nchini Tanzania.

Aliongeza kuwa ripoti ya mwaka 2021ya mwezi Septemba  iliyotolewa .na jarida la Afrika kuhusu hali ya ukatili wa kijinsia, Tanzania ni miongoni mwa wanandoa ambao ufanyiwa ukatili wa kijinsia.

" Asilimia 46 ya wanandoa hufanyiwa ukatili wa kijinsia, asilimia 36 walifanyiwa ukatili.  wa kimwili,asilimia 32 walifanyiwa ukatili wa kisaikolojia na asilimia 13 walifanyiwa ukatili wa kingono," alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na matukio ya kikatili kutokea kila mara,aliomba elimu ya Afya ya akili ianze kutolewa kuanzia shule za msingi hadi vyuoni.

Alisema Serikali iongeze bajeti kubwa katika afya ya akili kutokana na kutengwa kwa bajeti ndogo ya Afya ya akili.

" Kwa kuwa ugonjwa upo kwa jamii, Serikali inatakiwa iongeze bajeti hiyo,kiasi cha shilingi bilioni mbili kilichotengwa kwa ajili ya afya ya akili nikidogo kutokana na tatizo kuwa kubwa," alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...