Coolio, rappa mkali  wa Kimarekani aliyetamba miaka ya 90 na ambaye aliibua chati za muziki kwa vibao kama vile "Gangsta's Paradise" na "Fantastic Voyage," amefariki, rafiki yake na meneja Jarez Posey, amethibitisha.  Marehemu kafariki akiwa na umri wa miaka 59. 


Posey alisema Coolio alikufa Jumatano alasiri. Maelezo juu ya mazingira hayakupatikana mara moja. Ila Kapteni Erik Scott wa Idara ya Zimamoto ya Los Angeles alithibitisha kuwa wazima moto na wahudumu wa afya waliitikia wito kwenye Nyumba Namba 2900 block ya South Chesapeake Ave saa 4 asubuhi hiyo Jumatano kufuatia  wito za dharura ya matibabu. 


"Walipofika, walimkuta mwanamume aliyezirai na wakafanya “jitihada za kumfufua kwa takriban dakika 45. Ilishindikana. Mgonjwa huyo "alitangazwa kuwa amekufa kabla ya saa 5:00 usiku," Scott alisema.


"Tuna huzuni kwa kumpoteza rafiki na mteja wetu mpendwa, Coolio, ambaye amefariki mchana wa leo," taarifa  kutoka kwa meneja wa vipaji wa Coolio Sheila Finegan ilisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...