Na Pamela Mollel,Arusha
Vijana 130 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha wamefanikiwa kupatiwa elimu ya ujasiriamali pamoja na namna ya kujiajiri kwenye sekta ya viwanda
Vijana hao wamefanikiwa kupatiwa elimu kupitia mradi wa uanagezi ambapo mradi huo uliibuliwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia na kudhamiwa na Benki ya dunia Huku ikiratibiwa na SIDO
Akiongea na vyombo vya habari mapema jana mara baada ya kufungua mradi wa uanagezi ambao uliwakutanisha wamiliki,pamoja na vijana wajasiriamali mkoa wa Arusha meneja wa Sido mkoa wa Arusha Bw Jafari Donge alisema kuwa mradi huo ulidumu kwa kipindi Cha mwezi mmoja
Donge alisema kuwa Sido kupitia kwenye mradi huo umeweza kuibua ajira mpya kwa kuwa vijana hao waliweza kupelekea kwenye viwanda mbalimbali ambavyo vinatekeleza majukumu Yao ya kiujasirimali
"Vijana Hawa tuliwapeleka kwenye viwanda mbalimbali kama vile viwanda vya usindikaji,saluni,gereji,masuala ya mtandao,mikate,uhandisi,utalii Hawa wamiliki wote wapo chini ya Sido na tunashukuru sana wamewapokea kwa muda mfupi wa mwezi mmoja na tayari wameshapata mafunzo Huku wengine wakipata ajira za kudumu"aliongeza
Katika hatua nyingine aliwaasa vijana kuhakikisha kuwa wanatafuta fursa mbalimbali ambazo zinatangazwa ingawaje bado Kuna changamoto ya uhaba wa ajira
Pia aliomba wadau kama vile wizara husika kuweza kutoa fursa sanjari na kuibua miradi kama huo hata kama utadumu kwa muda mfupi ili kuweza kuwasaidia vijana kuanzisha na kumiliki viwanda vidogovidogo
Mmoja wa wamiliki wa viwanda Bi Salma mnaro aliweza kuishukuru waandaji wa mpango huo pamoja na Sido kwa kuweza kuwateua vijana ambao walikuwa na uitaji mkubwa wa ajira na hawana uwezo wa kupata uzoefu wa kumiliki viwanda
Salma aliongeza kuwa ni muhimu sana kuishukuru Serikali lakini pia Sido kwa kuwa wamekuwa matendo chanya ambayo wameweza kufungua milango kupitia hata taasisi za fedha
Alihitimisha kwa kuwataka vijana hao ambao muda si mrefu wanaanzisha viwanda vyao kuhakikisha kuwa wanasimama ipasavyo katika ndoto zao za kumiliki pamoja na kusimama katika ubora wa bidhaa ili waweze kuteka soko la dunia.
Meneja wa Sido Arusha Jafari Donge akizungumza katika mradi wa uanagezi ulioibuliwa na Wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia na kudhaminiwa na Benki ya dunia
Washiriki wa Mradi huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo
Mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza sabuni Salma Mnaro alipongeza serikali kwa kuja na mradi wa kuwezesha vijana kupata ajira
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...