NILIPOKUWA Shuleni nilisoma maana sahihi ya uzazi wa Mpango, nilielezwa na Mwalimu wangu kuwa ni uamuzi wa hiari unaofanywa na mtu binafsi,Mke au Mume au mwenzi wa kupanga ni lini wapate watoto na idadi ya watoto.

Sote tunafahamu kuna aina mbalimbali za uzazi wa mpango ambapo kuna Vidonge, Mpira ya kike na kiume,Sindano,Kalenda pamoja na zingine nyingi, lengo kubwa la kuwepo kwa uzazi wa mpango ni pamoja na kumwezesha mwanamke,Mwanaume kunufaika na haki ya uzazi ni lini wapate wataoto.

Umuhimu wa uzazi wa mpango ni njia sahihi na nafuu inayopewa kipaumbele hasa katika huduma za kinga za afya lakini pia ni muhimu katika kufikia malengo makuu ya afya hasa katika afya ya mzazi na watoto.

Siku ya uzazi wa mpango au World Contraception Day huwa huadhimishwa Septemba 26 kila mwaka hivyo lengo lake kubwa ni kuleta mkazo kwa haki za wanadoa wote na watu binafsi kuamua kwa uhuru na kuwajibika kuhusu idadi na nafasi ya watoto wao kupanga namna gani iwepo.

Pia, mashirika yasiyo ya kiserikali na yakiserikali,sekta binafsi,vyombo vya Habari na watu binafsi hukusanyika ili kuadhimisha siku hiyo kwa sababu bado kumekuwa na mitazamo hasi juu ya suala hilo na wengi hunda mbali Zaidi kuwa mtu akifundishwa uzazi wa mpango inaonesha kama anafundishwa kufanya ngono jambo ambalo siyo kweli.

Kwa mujibu wa UNFPA inalezwa kuwa Zaidi ya Wanawake na Wasichana bilioni1.8 Duniani wapo katika kundi la umri wa uzazi lakini wengi wo wanakabiliwa na vikazo pamoja n ukosefu wa taarifa na huduma za upangaji wa uzazi.

Sera ya Taifa ya Afya ya Mwaka 2007 ilisisitiza kuhusu dhamira ya serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi isiyolenga kupata faida na washirika wa maendeleo kuendelea kutoa huduma za afya bure kwa wajawazito, watumiajii wa huduma za uzazi wa mpango.

Aidha dira 2025 (Tanzania Bara)inaelezea mwelekeo wa Tanzania wa mpito kuanzia nchi inayoendelea hadi kufikia nchi ya pato la kati ifikapo mwaka 2025 ikitilia mkazo katika kuinua kiwango cha maendeleo ya binadamu na inaelezea umuhimu wa huduma bora za afya ya uzazi na kupunguza kiwango cha sasa cha vifo vya kina mama na watoto wadogo.

Wanawake wengi wanakuwa na watoto wengi kuliko mahitaji yao kwa sababu ya uwezo finyu wa kupata huduma ya uzazi wa mpango huvyo hupelekea baadhi yao kutofikia malengo.

Wapo baadhi ya wanawake bado hawajui nini maana ya elimu ya uzazi wa mpango .Takwimu za kituo cha Kimataifa cha Taarifa za Bioteknolojia NCBI cha marekani kinaeleza kuwa nchini Tanzania mwaka 2021 zinaonesha asilimia 27.1 ya wanawake wote walio katika umri wa kuzaa kwa sasa wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

Aidha kwa mujibu wa taarifa za UNFA inaeleza kuwa vifo vya uzazi Tanzania viliongezeka hadi vifo 556 kwa kila vizazi hai100,000 mwaka 2015 kutoka vifo 454 kwa kila vizazi hai100,000 mwaka 2010.

Siku moja niliwahi kuzungumza na baadhi ya vijana ambao kwa sasa ni waelimishaji rika maeneo mbalimbali na walisema wanakumbana na changamoto kutoka kwa baadhi ya wazazi wenye imani potofu kuwa kumpa elimu ya uzazi kijana ni kumhamasisha akafanye vitendo vya ngono.

Kwa majibu hayo, nilibaini wapo baadhi ya wazazi wanaoamini utoaji wa huduma rafiki kwa vijana ni jambo linalosababisha mimba za utotoni pamoja na maambukizi ya maradhi ya zinaa.

Tayari kuna wazazi au walezi wanawakatisha tamaa wanaotoa elimu kwa vijana hata ya kwenda kuelimisha shuleni au vyuoni kwasababu ya mawazo hasi.

Miongoni mwa wanawake niliokutana nao nikitaka kujua wanaufahamu kuhusu uzazi wa mpango Antonia masha anasema anakutana na watu wanaotoa elimu juu ya uzazi wa mpango lakini anaona aibu kuongea nao.

“Mimi natumia situmii uzazi wa mpango na nina watoto watatu ili wawili waliachana mwaka mmoja mmoja lakini nilijisikia vibaya laba elimu hiyo tuelimishwe mara kwa mara”anasema Antonia.

Siku ya uzazi wa mpango itakuwa inamchango mkubwa kwa jamii kwa sababu wapo baadhi ya wanawake wanashindwa kutimiza malengo yao na ndoto zao katika maendeleo endelevu.

Elimu ya uzazi wa mpango isichukuliwe kirahisi rahisi kwa sababu maendeleo hayawezi kuja bila ya kufata uzazi wa mpango,kwa sababu njia za uzazi wa mpango zinamchango mkubwa katika kupunguza mimba zisizotarajia.

Lakini pia,wanaume nao wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwakumbusha wake zao juu ya matumizi sahihi ya uzazi wa mpango ili waweze kuwa na familia bora yenye afya .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...