NA FARIDA MANGUBE. MOROGORO.

Waziri wa habari , vijana , utamaduni na micheza wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar mheshimiwa Tabia Mauled Mwita, amewataka wakurugenzi wa mashirika yanayoshiriki mashindano ya michezo ya bandari (Interport games) kuona uwezekano kwa mashindano ya mwaka 2023 kufanyika visiwani zanzibar kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi, umoja wa kitaifa na kudumisha muungano.


Waziri Mwita ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifungua mashindano ya 16 ya michezo ya bandari (Interport games) ambapo amesema wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Wizara ya utamaduni sanaa na michezo ya jamuhuri ya uungano wa Tanzania zimejipanga vyema kuhakikisha zinasimamia ipasavyo sekta ya michezo kwa pamoja ili kuleta ushindani katika michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.


“Niwatake washiriki wote mliopata fursa kushiriki mashindano haya mwende mkashindane na kuhakikisha mnafanya vinzuri na kupata ushindi wa pamoja, lakini vilevile kuna usemi unasema kushinda au kushindwa sio kitu cha msingi sana bali kikubwa kwenye mashindano haya ni kudumisha upendo,ushirikiano na umoja kwani sisi sote ni ndugu kwaiyo michezo hii isije kupelekea kutugawa badala yake tuendelee kuimarisha mmungano wetu .” Alisema waziri Mwita.


Akizungumza kwenye ufunguzi wa mashindano hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya bandari nchini TPA Plasduce Mbossa, Naibu Mkurugenzi Mkuu Bwana Juma Kijavala alisema TPA inatambua umuhimu wa michezo katika kuimarisha afya za wafanyakazi kwani mfanyakazi anapokuwa na afya njema hata utendaji wake wa kazi unaimarika.


“Ni sisitize tu kwa wafanyakazi wetu wote ni vyema kufanya mazoezi hata kama hakuna michezo hii ya interport.” Alisisitiza Bwna Kijavala
Alisema lengo la michezo hiyo ni kuongeza tija kwenye michezo ambapo aliwataka waamuzi wa michezo hiyo kutopendelea timu yoyote kwa masilahi binafsi kwani kufanya hivyo ni utovu wa nidham.


Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA Bi. Marim Mkama ameiomba serikali kuona kuwezekano wa mashindano hayo kufanyika mara mbili kwa mwaka ili kuongeza chachu ya ushindani kwa wanamichezo.


Mashindano hayo ambao yanafanyika kila mwaka na kwamba kwa mwaka huu yameshirikisha Taasisi nne za bandari zikiwa na timu tano ambazo zitacheza mpira wa miguu, mchezo wa kamba, riadha, pamoja na mpira wa kikapu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...