*Kwenye Mkutano wa Uwekezaji wa Sekta ya Mawasiliano

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
 
SERIKALI imesema inatarajia kuingia makubaliano na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ya kuunganishwa katika Mkongo wa Taifa wa Mwasiliano ili kuboresha huduma za mawasiliano nchini humo.

Hayo aliyasema Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kongamano la fursa za mashirikiano na uwekezaji katika sekta ya mawasiliano linalotarajia kufanyika nchini Congo kuanzia Oktoba 18-19, mwaka huu.

“Mbali na kongamano hilo, serikali ya Tanzania itaingia makubaliano na nchi ya Congo kuunganishwa katika mkongo wa taifa ili kuboresha huduma za mawasiliano kutaifanya nchi hiyo kuwa ya nane miongoni mwa nchi saba zinazotumia mkongo huo kwa sasa,” amesema.

Ameema nchi hiyo kutumia Mkono wa Taifa wa mawasiliano kutafungua fursa za kiuchumi na mapinduzi ya kidigitali kwa pamoja.

Katika hatua nyingine, Nnauye alisema kongamano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na waalikwa 300 na kampuni za 50 za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

“Tanzania tumekuwa tukifanya vizuri katika utoaji wa huduma za mawasiliano tofauti na nchi nyingine, japo bado kuna baadhi kuna changamoto lakini tumekuwa tukiendelea kuzitafutia ufumbuzi,” alisema.

Nnauye aliwataka wafanyabiashara kushiriki kongamano hilo kwa ajili ya kutangaza huduma za Tehama, kushiriki mijadala ya kukuza biashara, kujadili mashirikiano ya biashara na kutafuta fursa kuonesha ubunifu.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini, Kampange Gilbert amesema nchi ya Tanzania na Congo imekuwa na uhusiano wa muda mrefu.

Amesema wanaimani mkutano huo utaimarisha uhusiano uliopo na aliwakaribisha sekta binafsi na umma kushiriki kongamano hilo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Nape Nnauye akizungumza na waandishi habari kuhusiana mkutano wa uwekezaji wa Sekta Mawasiliano nchini Congo , jijini Dar es Salaam.
Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kampange Gilbert akizungumza kuhusiana uhusiano wa Tanzania na Congo kuendelea kuimarika katika masuala mbalimbali ikiwemo Tehama, jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...