NA.VERO IGNATUS,ARUSHA
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeweza kushiriki katika kusanyiko la Kisayansi la siku tano juu ya Udhibiti wa uhai wa dawa katika eneo la nchi za kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) lillofanyika Jjijini Arusha ,kupitia Mradi wa Maarifa ya Kesho.
Akizungumza Mkurugenzi wa Vifaa Tiba na Vitendanishi (TMDA) Kissa Mwamwitwa ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu amesema kuwa lengo la kusanyiko hilo ni kujadili mnyororo mzima kuanzia uzalishaji wa dawa,hadi utupaji salama na uondoaji wa kemikali za dawa katika mfumo wa maji taka mara dawa zinapomaliza muda wake na kuteketezwa.
Mwamwitwa alisema katika Kongamano hilo la Kisayansi waliweza kuangalia jinsi gani wanatumia maabara inayohamishika, katika kufanya uchunguzi wa kimaabara kuangalia ubora wa dawa ,hususani katika vituo vya forodha na katika ofisi za Kanda za TMDA,ambapo dawa yeyote inayoingia nchini wanachukua sampuli na kuweza kuangalia ubora
‘’Kwahiyo Mamlaka hii ya Dawa na Vifaa Tiba inawajibu mkubwa wa Udhibiti wa dawa,kuangalia ubora na ufanisi kabla hazijaingia sokoni na baada ya kuingia sokoni, wanamlinda Afya ya mwananchi na kuhakikisha wanatumia dawa zilizo salama na zenye ufanisi’’tukishajiridhisha na ubora ndipo dawa inaendelea kutumika pamoja na kuchukua sampuli, tunahakikisha kuwa bidhaa zote ni bora na zenye ufanisi kwaajli ya matumizi’’Alisema.Mwamwitwa.
Profesa Eliangirika Kaale ni Mtafiti kutoka Chuo Kikuu na Sayansi na Afya Shirikishi Muhimbili(MUHAS) : Tumeshirikishana uzoefu kutoka kwa kila mmoja wetu ambapo tumeona kuwa Mkakati wa kwanza ni kupunguza kusiwepo na dawa za kuharibu,kwa maana ya kwamba ni jinsi gani tutaepuka matumizi ya dawa ili mwisho wa siku kusiwepo na dawa nyingi ambazo zinabakia kwaajili ya kutupwa au kuteketezwa.
‘’Kwa upande wetu kwa sasa kuna changamoto kubwa ya safe disposal ya dawa kwasababu wadau mbalimbali hawajashirikishwa ,hivyo sisi kama watafiti wameona ni vyema wakawaleta kila wadau wanaohusika kwenye mnyororo huo wakiwemo walaaluma,wadau kutoka viwandani na Mamlaka za uthibiti’’.Alisema Kaale
Kaale:Tumekaa pamoja tukajadili kila mmoja wetu kwenye huu mnyororo kuanzia dawa iapoanza kutengenezwa mpaka dawa inavyotupwa ,na tumeweza kuja na mkakati kitu gani tunaweza kwenda kufanya ili kuhakikisha kwamba dawa ikishamaliza muda wake ni jinsi gani zitaharibiwa katika njia ambazo hazitaathiri mazingira
Kwa upande wake Prof.Peter Iming kutoka chuo Kikuu cha Martin Luther nchini Ujerumani,alisema amefurahishwa kuwa sehemu kusanyiko hilo la kisayansi la nchi za kusini mwa jangwa la Sahara SADC ,kwani wamefanya mjadala mkubwa ambapo utaleta matokeo chanya haswa kwenye uzalishaji,utupaji na uondoaji wa kemikali katika mfumo wa majitaka
Amesema wameweza kubadilishana uzoefu kutoka katika nchi mbalimbali na yeye kujumuisha na zile za nchini kwake na kuona kwamba mjadala huo umekuwa wa tija na umewaleta pamoja kuona namna ambayo wanaweza kutatua changamoto iliyopo kabla tatizo halijawa kubwa na kuleta madhara kwa mazingira na kwa binadamu.
Aidha warsha hiyo imefanyika August 29-septemba 3,2022
chini ya ufadhili wa Taasisi ya VW Foundationpamoja na mradi huo unaofahamika kwa jina la Maarifa ya Kesho(Knowledge for tomorrow), pamoja na miradi Shirikishi ya Tafiti katika eneo la nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.



Mkurugenzi wa Vifaa Tiba na Vitendanishi (TMDA) Kissa Mwamwitwa

Proches Patrick Meneja wa TMDA kanda ya Kaskazini akiwakaribisha wageni waliozuru katika ofisi hiyo ya. Kanda kujionea namna ambavyo atumia Maabara hamishika kutambua sampuli na ubora wa dawa


Titus Malulu Mataalam wa Maabara hamishika akitoa ufafanuzi kwa wageni waliotembelea Ofisi hizo kujionea namna Maabara hiyo inafanya kazi katika kutambua nnaiuangalia ubora wa dawa.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...