Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati wa NACOPHA kupitia Jukwaa la Vijana wanaoishi na VVU Tanzania (NYP+) mpango huo umefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF).
Mwenyekiti wa NACOPHA, Leticia Mourice Kapela akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo jijini Dodoma


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kasper Mmuya, amepongeza jitihada zilizofanyika kukamilisha uzinduzi wa mpango mkakati wa NACOPHA kupitia Jukwaa la Vijana wanaoishi na VVU Tanzania (NYP+) mpango huo umefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF).
Akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo jijini Dodoma, Mmuya amewataka vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi hivyo kwenye jamii zinazowazunguka.
Amesisitiza wadau wote wanaotekeleza shughuli za VVU/UKIMWI nchini kutumia miundo mbalimbali ya Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) zikiwemo Konga na vikundii wezeshi kutekelza shughuli zao.
Pia amekumbusha Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kuratibu vyema wadau wanaotekeleza afua za Ukimwi nchini. Pia ametoa mwito kwa vijana wote kujiunga na Bima ya Afya iliyoboreshwa ili kupunguza gharama za matibabu hasa ya magonjwa nyemelezi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa NACOPHA, Leticia Mourice Kapela amesisitiza upatikanaji wa huduma rafiki za VVU na Ukimwi kwa vijana wa umri balehe kwa ajili ya kujikinga na maambukizi mapya ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa Kondomu na pia uzazi wa mpango.
Pia amesisitiza utoaji wa elimu uongezwa katika jamii ili kupunguza unyanyapaa, ukatili wa jinsia na ubaguzi vinavyotokana na mila potofu hasa kwa wanawake na watoto WAVIU kupitia mwitikio wa viongozi wa dini na Taasisi zao.
Naye, Mwenyekiti wa mtandao wa vijana (NYP+), Pudensiana Mbwiliza ametoa wito kwa vijana kutetea uwepo wa mazingira wezeshi ndani ya jamii, na kujengewa uwezo ili kuongeza kujiamini miongoni mwa mwao wanaoishi na maambukizi ya VVU.
Pia amesema Kamati mbalimbali za vituo vya kutolea huduma za afya zishirikiane na vijana wanaoishi na maambukizi ya VVU kufanya tathmini ya maboresho ya mazingira rafiki ya kutolea huduma za afya kwa vijana, kutengeneza mipango ya maboresho, na kutekeleza mipango hiyo ili kuboresha huduma rafiki kwa vijana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...