Na Abdullatif Yunus Michuzi TV Kagera

Jamii imetakiwa kuona umuhimu wa kutoa Zawadi Kama Motisha na chachu ya kuinua Elimu katika maeneo yao, pindi pale Wanafunzi na Walimu wao wanapofanya Vizuri kitaaluma.

Akizungumza katika hafla ya Utoaji Tuzo na Zawadi kwa Walimu na Wanafunzi Waliofanya Vizuri Kitaaluma katika Kata ya Kanyangereko iliyopo Halmashauri ya Wilaya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jasson Rweikiza ameiomba Jamii kuiga mfano wa Wanajumuiya ya UMOKA ACADEMICS AWARDS wa Kuendeleza na kuboresha zaidi Utaratibu wa kutoa Zawadi kwa Washindi.

Dkt. Rweikiza Amesema kwa kufanya hivyo itakuwa Ni Namna nzuri ya kuwafanya Wanafunzi Kusoma kwa Bidii, na Walimu kufundisha kwa Bidii huku akisisitiza kuwa naye Kama Mbunge yupo mbioni Kuanzisha utaratibu wa zawadi Kama hizo kwa Jimbo Zima, huku akiahidi Kununua mashine za kuburuza Mitihani (Photocopier) kwa Jimbo zima, hii ikiwa ni moja ya Changamoto iliyobainishwa kwenye Risala iliyosomwa mbele yake akiwa Mgeni Rasmi.

Katika Hafla hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Ntoma, zimetolewa zawadi za Pesa, Medali na Vikombe, huku Mwanafunzi Godfrey Godwin kutoka S/M Ntoma akiibuka Mshindi wa Jumla wa Kata Kanyangereko, Mwl. Bora wa Masomo ya Sayansi, Hisabati, Kiswahili ni Mwl. Evelyna Leonard wa S/M Nyakabanga na Shule Kinara ni Shule ya Msingi Nyarubale.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...