Na Janeth Raphael
Wadau wa elimu nchini wanaoshiriki katika kikao maalum cha Menejiment ya Wizara na wadau wa elimu kutoa maoni ya kuboresha sera na mitaala ya Elimu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sekta hiyo muhimu Duniani.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda jijini Dodoma wakati akifungua kikao maalumu cha Menejiment ya wizara na wadau wa elimu kitakachofanyika kwa siku tatu kuanzia Septemba 26 mpaka 28,2022 jijini Dodomawa.
"Tuna kikao muhimu kwa mara ya kwanza tunakutana tukijadili tukiwa na Rasimu,moja Rasimu ya Mapitio ya Sera na pili Rasimu za Mitaala,kwa sababu kwa muda mrefu tumekuwa tukikusanya maoni,sasa tunakitu chakutumia kujadili na kazi hii kubwa alianzisha Rais wetu Tarehe 22 April 2022 alieleza bungeni kwamba tutajielekeza kufanya mapitio ya sera ya Elimu ya mwaka 2014 na kufanya marekebisho kwenye Mitaala iliyopo ili ielekeze kutoa Elimu ujuzi kulingana na mazingira ya nchi na soko la Ajira,ilikuwa ni Ahadi ya Rais Samia suluhu hassan kwa watanzani hivyo akatoa maelekezo tufanye kazi hii" Amesema prof Adolf Mkenda
Kwa upande wake naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali zanziba Ali Abdugulam Hussein amesema vijana lazma waandaliwe kitalamu na kiubunifu ili waweze kulitetea Taifa kimaendeleo na kushindana kimasoko.
"Tunatakiwa tujiulize kuwa inakuwaje mtoto mpaka anamaliza Elimu ya sekondari au chuo kikuuu hana ujuzi wowote na tegemeo lake apate ajira na tujiulize kuwa je kwa kiasi gani taaluma iliyotelewa inawajenga vijana wetu kuwa na nidhamu,uzalendo,upendo, mashirikiano na uzalendo wa kulilinda Taifa lao,haya ni miongoni masuala ambayo inawezekana kuna haja ya kuwafanyia Mapitio ya mitaala yetu ili kuimarisha upatikanaji wa Elimu bora itakayomsaidia kijana kukabiliana na changamoto za maisha yake na kuliletea Taifa Maendeleo kulingana na mabadiliko ya kiuchumi,kisiasa na kimazingira"Amesema Ali Abdugulam Hussein.
Dhima ya sera mpya na mitaala ya Elimu nchini ni kuinua ubora wa Elimu na Mafunzo na Kuweka Mifumo na Taratibu Zitakazowezesha Kupata idadi Kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikisha Malengo ya Maendeleo ya Taifa.
Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akizungumza katika kikao hicho jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Ali Abdugulam Hussein akizungumza leo Septemba 26,2022 jijini Dodoma wakati wa kikao maalumu cha Menejiment ya wizara ya elimu na wadau wa elimu kitakachofanyika kwa siku tatu kuanzia Septemba 26 mpaka 28,2022 jijini Dodoma
Sehemu ya washiriki wa kikao maalum cha Menejiment ya Wizara ya Elimu na wadau wa elimu kitakachofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...