Na Jane Edward,Arusha
Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amewataka wananchi mkoani Arusha kutunza miundombinu ya maji na kuacha kutupa taka ngumu kwenye miundiombinu hiyo.
Aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa mabwawa ya majitaka uliopo kata ya Terrat mkoani Arusha.
Msigwa alisema,kuwa kumekuwepo na changamoto ya wananchi kutupa taka nguvu kwenye mifuko ya miundombinu hiyo hali inayochangia wananchi kukosa maji kwa wakati kutokana na mifumo hiyo kuziba.
Aidha ameipongeza mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA) kwa namna ambavyo wameweza kuokoa shs 9 billioni katika mradi huo na hivyo fedha hizo kuweza kutumika katika
Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (AUWSA)Mhandisi Justine Rujomba amesema kuwa, mradi huo wa mabwawa ya majitaka umegharimu zaidi ya shs 15 bilioni na una uwezo wa kutiba majitaka lita milioni 22 kwa siku ndani ya miaka 20 huku mtandao wa maji taka ukiwa ni kilometa 268.
I
Mhandisi Rujomba amesema kuwa,baada ya miaka 20 ndo wataweza kufikiri teknolojia nyingine ya kutibu majitaka ,huku akitaka wawekezaji zaidi kujitokeza kwa kuwekeza zaidi katika mradi huo na kupitia majitaka hayo wameweza kutengeneza mkaa unaotokana na kinyesi cha binadamu na hivyo wamejipanga kupanda miti mbalimbali katika eneo hilo.
Amesema kuwa,kupitia mradi huo wameweza kujenga mabwawa 18 huku akimshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha hizo kwani wanajivunia kuweza kupata maji safi na maji taka na hivyo kupendezesha jiji la Arusha.
Mkurugenzi mtendaji wa AUWSA mhandisi Justin Rujomba,akizungumzia kuhusiana na mradi wa maji taka uliyopo Kata ya Terati Mkoani Arusha,aliyeko kushoto kwake ni msemaji wa serikali Bwn Gerson Msigwa.
Mhandisi Justin Rujomba akifafanua jambo kuhusu mradi huo katika ziara ya msemaji mkuu wa serikali Mkoani Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...